HABARI ILIYOTIKISA JIJI :CUF YATANGAZA VITA UCHAGUZI WA SERIKALI YA MITAA
Chama cha wananchi CUF kimesema patachimbika pamoja na damu
kumwagika endepo kama serikali itaendelea na vurugu na mchezo mchafu unaochezwa
katika maandalizi ya kuelekea chaguzi za serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika
mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari muda huu jijini dare s salaam
naibu katibu mkuu wa chama hicho bara bi MAGDALENA SAKAYA chama chake
kinasikitishwa sana na jinsi ya serikali ya chama cha mapinduzi kuvuruga
uchaguzi wa serikali za mitaa kwa makusudi kwa kuandaa machafuko kwa kutunga
kanuni mbaya isiyotekelezeka kanuni mwongozo mbovu wa uchaguzi huo.
Amesema kuwa hii ni dalili kuwa serikali ya chama cha
mapinduzi ilikurupuka katika kuandaa
uchaguzi huo na haikuwa na mpango kamilifu wa kufanya uchaguzi huo ndani ya
kpindi hiki kama ambavyo kumekuwa na kauli zinazokinzana kati ya Rais KIKWETE
pamoja na waziri mkuu MIZENGO PINDA kuhusu tarehe za kufanyika uchaguzi huo.*
Baadhi ya maneno ya kutisha yanayopatikana katika tamko laCUF LEO |
Akitaja mapungufu hayo ya uchaguzi huo ni pamoja na kutoa
mwongozo wa utekelezaji wa kanuni za uchaguzi ambapo maelezo yake yanakinzana
ambapo katika kanuni ibara ya 15 kifungu cha 1 kimejieleza vizuri na kutoa fursa
kwa mtiririko wa namna ya kuweka pingamizi hadi kujadiliwa kwa rufaa na kila
jambo limetengewa muda wake wa utekelezaji lakini katika mwongozo mtoririko huo
haupo badala yake unaelekeza maeneo mawili tu ambayo hayaendemio sambamba muda
wa kuwakilisha pingamizi kwa msimamizi msaidizi ambapo ni siku nne na muda wa kamati
ya rufaa kusikiliza rufaa ambapo ni siku nne na imetajana tarehe zake za
utekelezaji nov 26 hadi 29 lakini wakati huo huo hakuna muda wa kusikiliza
pingamizi hiyo kwa msimamizi msaidizi hakuna muda wa kukata rufaa kama
hujaridhika na maamuzi ya msimamizi msaidizi.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini
|
SAKAYA amesema kuwa malalalamiko hayo pamoja na mengine
mengi wamekwisha yafikisha katika ngazi husika na kamwe hawatakubali kuona wanachezewa
mchezo mchafu na kama serikli haitaacha mchezo huo patachimbika
Hakuna maoni
Chapisha Maoni