HABARI NJEMA JIJINI LEO-MABEHEWA MAPYA YAWASILI NCHINI,SASA TRL KUWA YA KISASA-SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka akikagua mabehewa mapya leo jijin Dar es Salaam |
NA Karoli
Vinsent
Serikali ya
Rais Jakaya Kikwete imedhamilia kuliboresha Shirika la Reli ya kati TRL ili
liweze kujiendesha lenyewe na kuacha kutegemea bajeti ya Serikali kwenye
mipango yak,baada ya leo kampuni hiyo imepokea Mabehewa 50 ya kubebea makasha
(Containres), ikiwa ni sehemu ya mradi wa serikali wa ununuzi wa mabehewa mapya
274 kutoka nchini India.
Kupokelewa
kwa mabehewa hayo, kunatarajia kuongeza kasi ya utoaji wa makasha ya mizigo
kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwa njia
ya reli kwenda nchi jirani za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na
Rwanda na kutimiza malengo ya Big result yaani matokea makubwa sasa.
Akipokea Mabehewa hayo leo Kwenye
bandari ya Jijini Dar es Salaa na kushuhudiwa na waandishi wa habari pamoja v,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka, alisema serikali inaendelea kutekeleza miradi 12 kupitia
Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN), yenye lengo la kuimarisha huduma ya
usafirishaji kwa njia ya reli.
Hapa ndipo Mahebewa hayo yakiwasili leo Jijin Dar es Salaam kwenye bandari |
Alisema
serikali imeshalipa zaidi ya bilioni 45 ikiwa ni gharama za ununuzi wa mabehewa
274 ambayo ni wastani wa milioni 166 kwa kila behewa.
Vilevile Katibu Mkuu huyo aliongeza
kuwa , lengo la serikali ni kuiwezesha TRL kusafirisha mizigo tani milioni 1.5
kwa mwaka na kuiwezesha kampuni hiyo kujiendesha kwa faida.
Vilevile
akatabainisha kuwa, baada ya kukamilika kwa mradi huo kutapunguza uharibifu wa
barabara kutokana na mizigo mingi kusafirishwa kwa njia ya barabara.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Mhandisi Kipallo Kisamfu, alisema katika
mabehewa 274 yaliyokwisha nunuliwa na
serikali yatakuwa ya aina tatu tofauti.
Alizitaja
ainia hizo kuwa ni mabehewa ya kubebea makasha, mizigo kichele na mafuta ambapo
ifikapo mwezi Februali mwakani, mabehewa yote yatakuwa yameshawasili nchini.
Mwezi Julai
mwaka 2011, serikali iliamua kuiendesha TRL baada ya mwekezaji kutoka kampuni
ya RITES ya India kubainika kushindwa kuiendesha kampuni hiyo kama
ilivyotarajiwa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni