Zinazobamba

SERIKALI YAOMBWA KUPUNGUZA KODI KWENYE VIWANDA NCHINI,SOMA HAPA ZAIDI

Na Habiba Chagamba.
Serikali ya Tanzania imeshauriwa kupunguza kodi za viwanda, ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa hapa nchini, na kusaidia ukuaji wa viwanda .
            Akizungumza na FULLHABARIBLOG  leo  jijini Dar e s salaam Mkurugenzi mtendaji wa BERGER PAINTS INTERNATIONAL  LTD  Bwana  

Mehbood  Bharwan amesema,   viwanda vingi vya hapa nchini vinashindwa kujiendesha kwa kuwa wanatoa kodi kubwa  serikalini tofauti na uzalishaji wa viwandani.
Bharwan amesema,  japokuwa serikali inahitaji kodi ili kuboresha huduma za jamii lakini kodi hiyo ni kubwa sana ambayo inatishia ukuwaji wa sekta ya viwanda hapa nchini

            “Utakuta kiwanda kinalipa kodi zaidi ya tatu wakati mmoja ambazo ni kodi katika mishahara , bidhaa na  katika usafirishaji  ambazo ni nyingi sana na katika mishahara tunakatwa 30% hiyo ni kubwa sana kwa upande wetu” alisema Bharwan
           Aidha amesema,  serikali itaweza kupunguza kodi viwanda vinaweza kuajiri watu wengi na kuzalisha zaidi na kuweza kusaidia kuinua uchumi wa nchi na wananchi kwa ujumla kwani kwa sasa wanashindwa kuajiri watu zaidi kwa kuwa uzalishaji wa bidhaa unakuwa mdogo na kodi ni kubwa.

             Mkurugenzi huyo amesema,  serikali inabidi iboreshe miundombinu ili kusaidia usafirishaji wa bidhaa, na  iweze kuboresha usafiri wa reli kwa ajili ya mizigo ili kupunguza gharama za usafiri wa bidhaa ambazo zitaweza kuwafikia wananchi kwa bei nafuu.

Maoni 2

Bila jina alisema ...

kwanza ana mashine za EFDs au analalamika huku akiibia serikali, pili huyo mhindi afaham hakuna nchi isiyokusanya kodi ili kuwaletea wananchi wake faida,

kwa taarifa yake sasa tunaanza kumchunguza uhalali wa ulipaji kodi kwa serikali

Bila jina alisema ...

aache usenge huyo muhindi, alafu wewe chagamba, mbona unaonekana unamsifia huyo kabachori wakati unajua wazi kuwa hao ni wazuri kwa kukwepa kodi, ona hata UBUNGO PLAZA imefungwa kwa kushindwa kulipa kodi hawa wahindi wanatufanya maendeleo yetu yarudi nyuma