ALIYETAJWA NA GAZETI LA MWANAHALISI KWENYE SAKATA LA DK ULIMBOKA APEWA UBALOZI SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
PICHANI NI SAED KUBENEA MMILIKI WA GAZETI LILOFUNGIWA LA MWANAHALISI KWA MDA USIOJULIKANA AKIONYESHA HABARI KWENYE MAGAZETI HAYO ILIYOPELEKEA GAZETI HILO KUFUNGIWA PICHA NA MAKTABA |
Jack Mugendi Zoka
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bw. Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada.
Bw. Zoka anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Alex Masinda, ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Zoka alikuwa Ofisa Mwandamizi Ofisi ya Rais Ikulu.
PICHANI NI Jack Mugendi Zoka |
IMETOLEWA NA
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Dar es Salaam,
Septemba 30, 2014.
Gazeti la MwanaHALISI liliandika yafuatayo kuhusu Zoka:
RAMADHANI Ighondu, afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ndiye ametajwa kuwa mtekelezaji wa mkakati wa utekaji wa Dk. Steven Ulimboka, MwanaHALISI limegundua.
Afisa huyo, licha ya kutambuliwa na Dk. Ulimboka mwenyewe, ndiye simu yake ilitumika kuandaa kikao ambako daktari alitekwa.
Ni afisa huyohuyo wa usalama ambaye alikutana na Dk. Ulimboka dakika chache kabla ya kutekwa.
Uchunguzi umegundua kuwa Ramadhani Ighondu (34), ni mfanyakazi wa ikulu aliyekuwa akifanya mawasiliano ya mara kwa mara na Dk. Ulimboka.
Ni mfanyakazi huyuhuyu ambaye Dk. Ulimboka amenukuliwa akisema, “...alinipigia simu na kuniita kwenye kikao ambako muda mfupi baadaye nilitekwa.”
Nyaraka nyeti ambazo mwandishi ameona zinaonyesha kuwa Ramadhani ndiye pia huitwa “Rama” – jina ambalo hutumia katika kujitambulisha na katika baadhi ya mawasiliano.
Rekodi katika simu ya Dk. Ulimboka: Na. 0713731610 zinaonyesha Rama ndiye alifanya mawasiliano ya mwisho na daktari huyo muda mfupi kabla ya kutekwa.
Aidha, ni Rama ambaye alikutana na kiongozi huyo wa Jumuia ya Madaktari Tanzania, maeneo ya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kutekwa.
Dk. Ulimboka alitekwa usiku wa 26 Juni, kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa  kucha na kutolewa meno; na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande.
Rama alifanya mawasiliano ya mwisho na Dk. Ulimboka saa 5: 52 kupitia simu yake Na. 0713 760473. Dokta alitekwa “muda mfupi” baadaye.
Rais Jakaya Kikwete aliliambia taifa kwa njia ya televisheni, mwishoni mwa Juni, kuwa serikali yake haihusiki na kuteka, kutesa na kutupa daktari porini.
Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliliambia bunge kuwa serikali yake haihusiki na utekaji na utesaji; na kuuliza, “...serikali imteke ili iweje?”
Mawasiliano katika simu ya Dk. Ulimboka yanaonyesha mtiririko wa simu za Rama wa ikulu hadi muda wa kutekwa katika eneo la Leaders Club.
Vyanzo vya taarifa ndani ya idara ya usalama wa taifa vinasema, kwa sasa Rama “amehifadhiwa” kwenye jengo moja la kificho linalotumiwa na idara hiyo lililopo eneo la Ada Estate, Kinondoni, Dar es Salaam.
MwanaHALISI limeweza kuthibitisha, kupitia vyanzo vya taarifa na nyaraka mbalimbali kuwa, simu Na. 0713 760473 iliyokuwa ikifanya mawasiliano ya mara kwa mara na Dk. Ulimboka, ni mali ya Rama.
Huyo ndiye Ramamadhani Ighondu (Rama). Mzaliwa wa Makole, Dodoma. Mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Idara hii iko chini ya Ofisi ya Rais (Utawala Bora) inayoongozwa na Rashid Othman.
Gazeti hili limepitia nyaraka mbalimbali, likiwamo daftari la kudumu la wapigakura lililoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kupata fununu zaidi juu ya tuhuma za Dk. Ulimboka kwa Rama.
Katika daftari hilo ambalo limetumika kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Rama anaonekana kujitambulisha kama ifuatavyo:
Ramadhani Ighondu,
Nickname: Rama
Born: 28.08.1978
Place: Makole Dodoma
Voter Registration Card: 49406879
Mobile Number: 0713 760473
Dk. Ulimboka ambaye anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini, amethibitishia MwanaHALISI kuwa mtu ambaye alikuwa anawasiliana naye mara kwa mara na kumuita kwenye mkutano maeneo ya Leaders Club, 26 Juni 2012, anatumia simu Na. 0713 760473.
Akizungumza kwa kujiamini Dk. Ulimboka amesema, “Ndiyo. Hiyo namba naikumbuka vizuri. Ni 0713 760473. Mwenye namba hiyo alikuwa akijitambulisha kwangu kwa jina la Abeid. Huyo bwana ndiye niliyekutana naye Leaders Club muda mfupi kabla ya kutekwa.”
Alipoulizwa anawezaje kukumbuka namba iliyokuwa inafanya mawasiliano na yeye wakati kipigo alichokipata kutoka kwa watekaji kilikuwa kikubwa hadi kupoteza fahamu, Dk. Ulimboka alisema:
“ Ninafahamu ninachokisema. Huyo bwana nilikuwa ninawasiliana naye mara nyingi na niliwahi kukuta naye katika mgogoro ule wa kwanza wa madaktari.”
Kauli hii ya Dk. Ulimboka inafanana na ile aliyoitoa kabla ya kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu, 30 Juni 2012.
Katika mahojiano yake yanayopatikana kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, Dk. Ulimboka anasema, “Huyu bwana kwa muda wa siku tatu mfululizo alikuwa anajaribu kuwasiliana na mimi lakini kwa bahati mbaya ratiba yangu ilikuwa haiwezekani kumuona.
“Nilishawahi kukutana naye kwenye mgogoro ule mwingine, lakini this time of course (mara hii) alikuwa serious (makini) akinitafuta…Huyu bwana anafanyakazi ikulu.”
Katika mahojiano hayo, Dk. Ulimboka anasisitiza kuwa wakati anatekwa alikuwa na akili timamu na hivyo anamfahamu aliyemteka kuwa ni mtu kutoka ikulu.
Dk. Ulimboka anasimulia “mtu wa ikulu” alivyoingia kwa gari pale walikomwambia wameketi na kumuuliza iwapo alikuwa na Deo (Dk. Deogratias Michael) na kwamba walianza majadiliano yaliyohusu hali ya mgomo na jinsi wao walivyokuwa wakiona unaweza kutatuliwa.
“Sisi tukasema mambo yote yanafahamika. Tukaongea naye kwa muda mfupi tu; akawa anaandika… kwa hiyo pia alikuwa very busy communicating, (akionekana kujishughulisha zaidi na mawasiliano ya simu). Unaona?”
MwanaHALISI limegundua kabla ya Dk. Ulimboka kutekwa, Rama alianza kufanya mawasiliano naye saa 12: 25 jioni. Mawasiliano hayo yaliendelea 3:29 usiku, saa 4: 52, saa 5: 27, saa 5:40 na mwisho ilikuwa saa 5:52 usiku.
Haya ndiyo mawasiliano ambayo Dk. Ulimboka aliishasimulia kuwa yalielekea katika kukutana kwake na mwenye simu Na. 0713 760473. Ni mwenye simu hii aliyeandaa mkutano, anakumbuka Dk. Ulimboka.
Kabla simu ya Rama kumwita Dk. Ulimboka kwa mara ya kwanza siku hiyo, saa 12:25, ilifanya mawasiliano na Buruani Ntilongwa, mmiliki wa simu Na. 0712 359533.
Mawasiliano hayo yalifanyika kati ya saa 2: 08 na 2: 24 usiku.
Aidha, nyaraka zinaonyesha kila pale Rama alipowasiliana na Dk. Ulimboka, alifanya mawasiliano pia na
Moshi Marungu Shabani anayemiliki simu Na. 0761 132663 na 0655 162663.
“Nakwambia ndugu yangu, kila pale ambapo Rama alifanya mawasiliano na Dk. Ulimboka, utaona hapohapo alifanya mawasiliano na Abdallah Kunja na Ntilongwa. Hawa ni watu muhimu sana kwenye sakata hili,” taarifa zimeeleza.
MwanaHALISI limegundua kuwa siku mbili kabla ya Dk. Ulimboka kufanyiwa unyama huo (24 Juni 2012), simu ya Rama iliingizwa salio la Sh. 252,849. Hili ni salio kubwa pekee kuingizwa kwenye simu hiyo tangu mwanzo wa mwaka huu.
Nyaraka zinaonyesha tarehe 4 Mei 2012 simu ya Rama iliwahi kuishiwa salio kabisa hadi kufikia kiwango cha Sh. 1.
SOURCE MWANAHALISIFORUM
Hakuna maoni
Chapisha Maoni