SAKATA LA UTEKAJI WA WATOTO DAR,KAMANDA KOVA AUNGURUMA ASEMA UKWELI WA MAMBO NA KUHUSU JAMBAZI SUGU KUKAMATWA SOMA HAPA
Na Karoli
Vinsent
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekanusha vikali juu ya uvumi
unaoendelea jijini Dar es Salaam kuhusu utekaji nyara wa watoto wadogo
wanaosoma shule.
Kutokana
na Hivi karibuni umezuka uvumi kutoka kwa watu mbalimbali hasa wazazi ambao
uvumi huu umewafikia kwamba kuna kundi la wahalifu wanaotumia gari aina ya NOAH
rangi nyeusi ambao kazi yao ni kuteka nyara wanafunzi kwa nia ya kutenda
uhalifu ikiwa ni pamoja na kuwachuna ngozi na madhara mengine.
Akikanusha Taarifa hizo leo Jijini Dar
es Salaam na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar Es Salaam Kamishna Suleiman Kova
wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo alisemaMpaka sasa Jeshi la
Polisi halina taarifa yoyote ya mtoto kutekwa au kufanyiwa madhara yoyote kwa
mtindo wa utekaji nyara.
Pia, Jeshi la Polisi limegundua kwamba huu
ni uvumi ambao haujulikani chanzo chake hivyo wananchi wanaombwa kuachana na
uvumi huo na kuupuuza kwani unaleta hofu katika jamii bila sababu za msingi.
Aidha, uvumi huu umeanza kuleta usumbufu
ambapo mnamo tarehe 03/10/2014 saa tatu asubuhi huko vingunguti mtu mmoja
aitwaye PROSPER MAKAME miaka 34, mfanyakazi wa The Guardian Ltd, mkazi wa
Tabata akiwa na mkewe MARYSTELLA MUNIS, Miaka 30, mfanyabiashara wa vyombo vya
nyumbani walifika maeneo ya shule ya msingi Kombo iliyopo Vingunguti kwa ajili
ya kuchukua pesa za vyombo wakiwa na gari aina ya NOAH yenye namba T252 DAY
rangi nyeusi. Ghafla walikuja watu wanaokadiriwa kufikia mia moja (100) na
kulizingira gari hilo kwa makelele wakidai kuwa ndilo linalowateka wanafunzi.
mtoa taarifa alipoona hali inakuwa tete alipiga simu Polisi na hatimaye watu
hao waliokolewa na Polisi kisha kufikishwa katika kituo cha Polisi Buguruni
wakiwa salama pamoja na gari lao.
Pia
mnamo tarehe 13.10.2014 majira ya saa 10:00 hrs huko katika kituo cha polisi
Tabata uliibuka uvumi kuwa gari namba T548 BUN aina ya Noah rangi nyeusi ambayo
ni mali ya askari polisi aitwaye A/INSP ESTAR wa kikosi cha usalama barabarani
kituoni hapo ndani yake kuna vichwa vitano vya watoto wa shule ya msingi
Mtambani na kusababisha wazazi wa watoto wanaosoma shuleni hapo na wananchi
wengine kukusanyika kituoni hapo ili kushuhudia na kuona hivyo vichwa vitano,na
ndipo mkuu wa kituo hicho cha Polisi Tabata aliamuru gari hilo kufunguliwa na
kuwathibitishia wananchi kuwa habari hizo ni za uwongo na uvumi.
Vilevile Jeshi la Polisi Kanda Maalum
Dar es salaam linasisitiza kuwa uvumi huu wa kuwepo kwa kikundi cha wahalifu
ambao wamekuwa wakiwateka watoto/wanafunzi hao si wa kweli hata kidogo na hivyo
wananchi wanatakiwa kuepukana na taarifa hizo ambazo kwani zinaweza kusababisha
uvunjifu wa amani.
Aidha,uchunguzi
wa kubaini ni nani aliyeeneza uvumi huo ulifanyika na kubainika kuwa uvumi na
habari hizo zimeenezwa na mtu aitwaye GILBERT s/o STANLEY,(32) mhehe,mkulima,na
mkazi wa Tabata ambaye alikamatwa muda mfupi tu baada ya tukio hilo na
alipohojiwa alikiri kweli kueneza habari hizo na yeye aliambiwa na mtu mwingine
ambaye hata hivyo alisema hamkumbuki.
Katika Hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda maalum
ya Dar es salaam kupitia makachero wa
kikosi kazi mkoa wa Kinondoni(Task Force)_mnamo tarehe 14/10/2014 majira ya saa
06:45 hrs huko Chanika (W) Ilala lilifanikiwa kumkamata jambazi sugu aitwaye
Paulo s/o Thomas Milanzi @Chinga,mmakonde,mkristo,hana
kazi,miaka 35,mkazi wa Chanika.Kabla ya ukamataji jambazi huyo alianza
kuwashambulia askari polisi kwa kufyatua risasi kwa bastola huku akikimbia na hatimaye
askari polisi walijibizana nae na kumjeruhi kwa risasi maeneo ya mgongoni na
baadaye kumkimbiza hospitali ya taifa Muhimbili kwa matibabu na baadaye
madaktari walithibitisha kuwa amefariki.
Aidha jambazi huyo
alikuwa akitafutwa na polisi kwa muda mrefu kuhusiana na matukio mbalimbali ya
mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha jijini Dar es salaam na mikoa ya
jirani.
Baadhi ya matukio aliyowahi
kufanya jambazi huyo ni 1. Tukio la tarehe 29/04/2014 lilitokea huko Airport
kwenye taa za kuongozea magari akiwa na majambazi wenzake ambapo walimuua kwa
kumpiga risasi Ofisa mwandamizi wa Usalama wa taifa SYLIVANUS s/o ADRIAN MZERU
na kupora kiasi kikubwa cha fedha,2.Tukio la mnamo tarehe 21/02/2014
lililotokea maeneo ya Oysterbay katika barabara ya Haille sellasie karibu na
Jackies Bar ambapo walivunja kioo cha gari aina ya Nissan Patrol iliyokuwa
inaendeshwa na SYLIVANUS s/o ADRIAN MZERU na kupora pesa taslimu na laptop
computer na wakati wanakimbia walimuua kwa kumpiga risasi ubavuni mlinzi wa
kampuni ya KK security aitwaye FRANK s/o SILAYO,3.Tukio la mnamo tarehe
17/02/2014 lililotokea Kinondoni studio akiwa na wenzake ambao walishakamatwa
wakitumia usafiri wa pikipiki walimvamia mfanyabiashara LUKAS s/o MONGI ambapo
walifyatua risasi hewani kwa silaha walizokuwa nazo ambazo ni SMG na Bastola
mbili kisha kumpora kiasi cha shilling 20,000,000/=.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni