HOMA YA MECHI KATI YA SIMBA NA YANGA.KAMANDA KOVA ATOA ONYO KALI KUHUSU MECHI HIYO
Na Karoli Vinsent
Jeshi la Polisi Kanda Maalum limejipanga vyema
kuimarisha ulinzi wakati wa mechi ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi
ijayo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam.
Akithitisha hali ya Usalama wakati wa Mechi
hiyo,Kamishna wa Kanda Maalum ya Polisi ya Dar Es Salaam, Suleiman Kova Wakati
wa Mkutano na Waandishi wa Habari Leo Jijini hapa,ambapo Kova alisema Mashabiki
wanatakiwa kukaa katika sehemu zao kadiri ya tiketi walizokata
Pia Kova aliongeza
kuwa ni marufuku kwa mashabiki kuingia
na silaha aina yoyote kwa mfano chupa za maji na kusema Mageti rasmi pekee
yatumike kuingia uwanjani na CCTV Camera zitatumika kuangalia na kutunza
kumbukumbu kwa matukio yoyote yatakayojitokeza kabla, wakati na baada ya
mchezo.
Vilevile Barabara
zote zinazopita uwanja wa Taifa zitafungwa kwa muda mpaka yatakapotolewa
maelekezo mengine,
Aidha,Vitengo mbali mbali vya Polisi vitatumika
kuhakikisha kwamba Amani na Utulivu vinatawala wakati wote wa mchezo huo. Mashabiki wanatakiwa kuwa watulivu wakati
wote wa mchezo na waheshimu maamuzi ya mwamuzi na utii wa sheria bila shuruti.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni