BUTIKU-KWA UCHAFU HUU WA CCM BASI WANAMIAKA KUMI TU YA KUKAA MADARAKANI,SOMA HAPA KUJUA
Kada mkongwe wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Joseph Butiku, amekionya chama chake kuwa kama hakitaachana na
mwenendo wake wa sasa, uwezekano wa kuwapo miaka 10 ijayo ni mdogo.
Katika mahojiano
maalum na Chanzo chetu ofisini kwake jijini Dar es Salaam ambayo alizungumzia
mambo mbalimbali wiki iliyopita, Butiku alisema chama hicho kimejiengua kwenye
misingi yake kwa kiwango kikubwa, huku vitendo vya rushwa vikikumbatiwa katika
kusaka uongozi wa nchi.
“Si lazima iwepo (CCM), lazima ibadilike. Irudi iwe CCM. Isipobadilika haitakuwa CCM kwa sababu ukiacha kusimamia misingi, itakuwapo hewa. Upepo ukiisha kwenye mpira hata wa gari, inasimama,” alisema na kuongeza:
“Wanachama tunaoijua CCM ilivyokuwa sivyo ilivyo leo. Na sioni aibu kusema hivyo. Mimi ni mtu mzima sasa, nimekulia ndani ya CCM. Naijua, najua gharama ya kuwa mwanachama na kiongozi wa CCM ni kujitoa kwa kiwango cha juu kabisa kuwatumikia watu, sivyo ilivyo sasa.”
Alisema CCM ina katiba na miongozo mizuri, lakini haiheshimiwi na kwamba watu wanadiriki kuvunja robo tatu ya misingi ya chama bila kuchukuliwa hatua na kufanya hivyo kunahatarisha uhai wa chama.
“Mimi sina aibu kusema. CCM ina katiba ambayo ina historia na ina miongozo. CCM siyo mimi Butiku, ni ya wanachama. Ukivunja zaidi ya robo tatu ya misingi hiyo, unabaki ni CCM (kweli)?” alihoji.
Butiku alisema: “CCM ilikuwa inasimamia utu, usawa, heshima, haki, uhuru wa Watanzania. Imesimamia watu wapate elimu, imeweka mfumo wa demokrasia ya kuchaguana kuanzia juu hadi chini. Lakini hivi sasa, leo CCM katika uchaguzi, haki imekwisha kabisa... ni rushwa.”
“Ukishaweka rushwa, ile waliyosema rushwa kwetu mwiko, umeshavunja heshima, haki, utu na umeondoa uhuru. CCM sasa ina mwelekeo wa kuwa chama cha mabavu. Ni aibu kwa sababu hatujawahi kuwa chama cha mabavu,” alisema.
Aliongeza kuwa: “Hatujawahi kusambaza polisi kila mahali kulinda watu wetu, walikuwa wanajilinda hata wakati wa kudai uhuru. Tulikuwa na maadui wa nje wengi, lakini tulitegemea watu wetu.”
Butiku ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere aliyekuwa pia mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema alishawahi kueleza kuwa CCM imepoteza mwelekeo, lakini chama kikamkosoa.
Hata hivyo, alirudia kauli yake kwa kusisitiza kwamba 'CCM inazidi kupotea'.
“Na leo narudia, CCM inazidi kupotea... kilichotusaidia ni katiba yetu na uongozi uliosimamia utekelezaji wa katiba hii pamoja na ile ya nchi. Leo CCM inaweza ikavunja katiba na isijali.”
WANAOTAJWA URAIS CCM
Bila kutaja majina ya watu waliojitangaza kuutaka urais kupitia CCM, Butiku alisema kuwa miongoni mwao haamini kuwa yupo mwenye sifa thabiti za kushika wadhifa huo.
Butiku ambaye alikuwa Katibu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa takriban miaka 21 alisema: “Frankly (ukweli), wanaosema wanautaka (urais), wote hawana sifa ya kuwa rais. Nikipata nafasi nitawaambia kwa sababu nawafahamu.”
Alidai kati ya wale waliojitangaza, haoni yeyote kati yao mwenye uwezo wa kutetea kwa dhati maslahi ya wananchi kama utu wao, heshima, ardhi yao na kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinawanufaisha Watanzania wote.
SIFA ZA RAIS
Akizungumzia sifa za rais, Butiku alisema kwa mtazamo wake, anaamini kuwa yeyote anayetaka urais ni lazima awe ni mtu anayetambua majukumu ya taasisi hiyo na kukubali kuyabeba kwa nia ya kulisaidia taifa na siyo kujinufaisha binafsi.
“Nyerere alituambia mtu anayetambua uzito wa urais si mtu anayeshabikia urais kama cheo. Ni mtu anayetambua uzito wake na kusema pamoja na uzito huu, mimi nitabeba (jukumu), nitasaidiana na wenzangu kuona kwamba umaskini unaondoka, afya ni nzuri zaidi na mambo mengine,” alisema Butiku.
Alitaja sifa muhimu ya pili kuwa ni lazima mtu anayekuwa rais awe ni mwadilifu, anayeheshimu watu wote na ambaye anawapenda watu wake kama anavyojipenda mwenyewe
Alisema kuwa kamwe haiwezekani mtu kushika wadhifa huo ikiwa hawapendi watu wake.
Akifafanua, alisema kumheshimu mtu na kusimamia haki na usawa ni masuala yasiyo na mjadala na hivyo, ni mambo ya msingi ambayo kiongozi mkuu wa nchi anapaswa kuwa nayo.
Sifa ya tatu, kwa mujibu wa Butiku, ni kwamba rais asiwe mtu mwenye kupenda kujilimbikizia utajiri. “Huwezi kuwa rais halafu ukahangaika mno na utajiri wako binafsi. Rais anapaswa amudu presha (shinikizo) ya ndugu zake, marafiki zake, watoto wake na mke wake...ukikaa pale wakuone umekaa rais na siyo baba. Uko wakati wa (kuwa) baba na wakati wa (kuwa) baba wa wote," alisema.
Alisema: “Ukikaa watoto wako wajue umekaa pale kama baba wa wote... siyo baba wa kutafutia kazi (watoto) kwa magendo.”
Akimzungumzia Mwalimu Nyerere ambaye kesho ni kumbukumbu yake ya miaka 15 tangu alipofariki dunia Oktoba 14, 1999, Butiku alisema alikuwa ni kiongozi ambaye Watanzania na dunia nzima, wanaendelea kumsifu kwa sababu alisimamia utu na heshima, usawa na uhuru bila kujali cheo au udogo wa mtu
pichani Ni Joseph Butiku |

Chanzo Ni
gazeti la Nipashe
Hakuna maoni
Chapisha Maoni