Zinazobamba

YALIYOSEMWA NA MECK SADIKI SASA YATIMIA, WAKAZI DAA WALALA JUU YA MAJI








HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MECK SADIKI,

Kile kinachoonekana kama liwalo na liwe, leo hii mkuu wa mkoa wa Daresalam amtaka rasmi kuwa serikali yake haitawajibika kwa matatizo yoyote yatakayojitokeza kwa wale wananchi wanaokaa mabondeni, na zile sehemu hatarishi ambazo uwezekano wa kukubwa na mafuriko ni mkubwa na kwamba yeyeote atakayengoja mafuriko yamkute ndipo aanze kulaumu serikali,hiyo itakuwa ni kazi ure,
Tunamsikiliza, baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia mkutano wake mapema hii leo wakiwa makini kuchukua habari, ili kuwapasha habari wananci, Meck Sadiki amesema serikali imedawa juu ya kadhia ya wananachi wanaoishi mabondeni, sababu kubwa ya kunawa ni kutokana na wananchi kwenda mahakamani kudai haki zao

Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Daresalam, Mkuu huyo wa Mkoa amesema hatua imekkuja kufuati wakazi wa maeneo hayo kukaidikuondoka kwa hiari na hata serikali ilipotaka kuwaondoa kinguvu bado wamekuwa wakaidi na kuamua kufngua kesi mahakamani wakiitaka mahaka kuweka hati ya zuio ili wasieze kufukuzwa katika maeneo yao,

Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini, mkuu wa mkoa wa Daresalaam akifafanua jambo mbele yao.
Sadiki ameongez kusema kuwa sasa hakuna msalie mtume, Tatizo lolote litakalojitokeza katika mabonde hayo watajua wenyee wapeleke wapi vilio vyao kwani sasa serikali imenawa mikono kuhusiana na kadhia hiyo
Ameongeza kusema kuwa, wananchi wafahamu kuwa serikali haina nia ya kuingilia muhimili mwingine wa serikali kwa kuwafukuza maeneo yao yanayokaa, lakini wafahamu kuwa serikali haitakuwa pamoja kwa madhala yoyote yatakayojitokeza.
Mkuu wa mkoa wa Daresalaam akisikiliza moja ya maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na kunawa kwa serikali kuwasaidia wakazi wa mabondeni katika mafuriko yaliyotabiriwa,
 Kama unavyojua Tayari mamlaka ya hali ya hewa imeshatoa angalizo kuhusiana na mvua zinazoendelea jiji Dresalaam , hivyo watu wa mabondeni ni vyema wakatoka wenyewe kuliko kungoja mpaka mafuriko yawafunike ndipo unakumbuka kuhama, na huko hakuna na tofauti na kukumbuka shuka wakati kumeshakucha
A idha katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa Daresalaam amewataka wakazi wa Daresalaam kuhudhlia katika sherehe za siku ya mwanamke ambayo itafanyika march 8 pale mwembe yanga, huku mgeni rasmi akiwa waziri wa jinsia na watoto.
Meck Sadick amesema kuhudhulia kwa wananchi ndio kufankisha kwa sherehe hizo, hivyo i vyema wakatumia muda wao kuja kusherehekea kwa pamoja siku ya mwanamke ambayo kwa mwaka uu inakaul mbiu nzuri inayochochea kuheshmiwa kwa haki za mwanamke hapa nchini



Hakuna maoni