JUKWAA LA KATIBA LASIKITISHWA NA HUTUBA YA JK BUNGENI DODOMA, LASEMA AMEHARIBU MCHAKATO MZIMA WA KATIBA
Waandishi wa habari, wakiwa makini kuchukuwa taarifa ya kaimu huyo, hata hiyo, mwenyekiti huyo hakusita kusali ya hewa na ndio maana mpaka sasa, bunge halijatulia tokea kutolewa kwa hutuba yake |
JK ameanzisha mchakato wa katiba mwenyewe na ameharibu
mchakato wa katiba mwenyewe, hayo si maneno yangu ni maneno ya makamu
mwenyekiti wa jukwaa la katiba Mh. Hebroni Mwakagenda wakati anatoa taarifa
yake kwa waandishi wa habari kuhusiiana na sintofahamu inayoendelea katika
bunge la katiba huko Dodoma,
Akizungumza na waandhis wa habari mapema hii leo, Mwakagenda
hakusita kuonyesha masikitiko yake kwa mkuu wan chi kwa kitendo chake cha
kuharibu mchakato wa bunge la katiba na kusema kwamba bunge hilo likivunjika
hakuna wa kulaumiwa zaidi ya mkuu huyo wanchi aliyeharibu mchakato huo kwa
makusudi,
Mchakato wa kuipata katiba mpya ulikuwa ukienda vizuri
kabisa, lakini kitendo cha Mh. Raisi kuonyesha hisia zake katika Bunge hilo,
bunge hilo limeshindwa kutulia kabisa na hakuna mtu yeyeyote wa kulaumiwa zaidi
ya mkuu wan chi,
Haiingi akilini hata
kidogo kuwa mapendekezo ya katiba kuwa
yali kuwa ni mageni machoni mwa raisi mpaka asubiri hadi siku ya mwisho ndipo
akamzalilishe mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba, Jaji Joseph Sinde walioba
pale Bungeni, Aliongeza Mwakagenda,
Tunafahamu kuwa rais haikuwa nia yake kumzalilisha
mwenyekiti wake alimpa fulsa ya kukusanya maoni ya wananchi na kuyawasilisha
kwake halafu hatua za mwisho rais anaibuka na kusema kuwa Rasimu inamapungufu
makubwa sana , kwani mapungufu hayo hajayaona mpaka asuburi siku ya mwisho
ndipo akamzalilishe mzee wetu jaji Sinde Walioba,
Tunaamini kuwa hilo linaweza kuwa ni shinikizo, na ndipo
maana baada ya kusomwa kwa hutuba ile ya rais , watu walifanya sherehe hadi saa
saba za usiku wakisema tayari wameshamaliza mchezo na kwamba kila kitu kinaenda
kama kilivyopangwa,
Mchezo huu mchafu haukubaliki hata kidogo na kwamba juu kwa
la katiba Tanzania tumedhamilia kuhakikisha kuwa mchakato hautoki nje ya njia
kuu, na kwamba kama inaonekana watu Fulani wanakazania maslahi ya chama Fulani,
hawatasita kwenda bungeni kulifunga bunge hilo,
Akifafanua mbinu zitakazotumika kulifunga bunge hilo,
Mwakagenda amesema ni mapema mno kusema njia itakayotumika kulifunga bunge hilo
na badala yake siku ikifika watawaambia wananchi kwenda kule Dododma kulifunga
bunge hilo.
Akizungumzia suala la upigaji wa kula, Mwakagenda hakusita
kuonyesha msimamo wa JUKATA kuwa wanaona ni vyema kura ya sili ikatumika kwani
duniani kote kitu kinachoitwa kura ni siri,na kwamba kitendo cha kuruhusu watu
wapige kura ya wazi ni sawa na kumlazimisha mtu abadili malengo yake kwa
kuogopa mtu Fulani kutokana na cheo
chake,
Angalia pale bungeni, watu wako na bosi wao, kama bosi wako
ametaka serikali mbili wewe ni nani hasa ukakataa serikali hiyo mbili, kuna
mawazili, naibu waziri hivi ni nani hasa atakaekuwa na ujasili wa kukataa
mapendekezo ya mkuu wake wa kazi, tusidanganyane hata kidogo hakuna hata mmoja
atakaekuwa tayari kumpinga bosi wake anayemfanya aweze kuendesha maisha yake,
Kura ya siri ni muhimu kama kweli tunataka katiba yenye
kumstawisha mtanzania na siyo vyma Fulani hapa nchini,
Hivi ni kwanini watu wanaogopa kupiga kura ya siri, kuna
nini hapa???, mbona kumchagua mwenyekiti wa bunge hilo ilitumika kura ya siri, nap
engine swali linguine la kizushi , ni utaratibu gani ama ni kura gani itatumika
kupiga kuwa ni kura gani itumike kati ya kura ya siri ama kura ya wazi,
tusidanganyane, nadhani kura ya siri itatumika basi vivo hivyo kura ya siri itumike
kupitisha katiba hiyo,
Kwani nao wananchi watatumia kura ya mtindo gani kupitisha katiba
bila shaka ni kura ya siri, sasa kunaukakasi gani kwa wabunge wetu kutumia kura
ya siri kuamua mambo mazito kama haya, ama kunawatu wanaajaenda binafsi hapa,
tunaema hatutokubali hata siku moja fedha za mlala hoi zikatumika kuwanuafisha
maslahi ya watu wachanche, aliongeza Ndg Islae Ilunde, mmoja wa wajumbe
machachari wa jukwaa la katiba,
Naye Kaimu mkurugenzi wa mtandao wa mashirika yanayotoa
masaada wa kisheria Tanzania na mjumbe wa kamati ya ufundi JUKATA, Bw. Gorge
Mollel ameweka wazi suara ya kura ya
siri, akisema hakuna namna ya kuiepuka kura ya siri kwani katika hatua zote za
upitishaji wa mchakato huo unahitajika kura ya siri kuanzia kwa wananchi
wenyewe na hata wabunge,
Kuogopa kura ya siri ni ishara kuwa kuna watu wanaajenda yao
ya siri,na kubainisha ni vigumu sana watu kupiga kura ya wazi kwani kura hiyo
itatawaliwa na woga kwa wajumbe wa bunge la katiba
Mpaka sasa bunge hilo limeshatumia jumla ya fedha halali ya
kitanania Bilioni 80, huku mambo bado yakiwa hayajatulia hata kidogo tokea
hutba ya mkuu wan chi kuharibu hali ya hewa huko mjinii Dodoma, na kuna mashaka
makubwa yametanda kama safari ya kupatikana katiba mpya itafanikiwa, swali
kwako Mtanzania kama tumetubia mabilioni tote hayo kwa hasra nani anastahili
kuwajibika katika hilo, mimi simo,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni