KONGAMANO KUBWA KUFANYIKA DAR, WAKULIMA WAFANYABIASHARA WAKUBWA WATAKIWA KUKAMATA FURSA ZILIZOO, ZAIDI SOMA HAPAA
DAR ES SALAAM
Wafanya biashara na wakulima
wametakiwa kutumia furusa mbalimbali zinazotokea hapa nchini kwani zitawasaidia
katika kukuza na kuendeleza uwezo wa kibiashhara na kilimo hatua ambayo
itawafanya wazidi kukua kiuchumi na kufika katika masoko ya kimataifa katika
biashara zao.
Akizungumza leo jijini dare s
salaam Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Kigdom Leadrship Network Tanzania
Mheshimiwa IBRAHIM KADUMA amesema wafanya biashara wanaweza kunufaika zaidi
kutokana na shughulizao kama wataweza kutumia furusa mbalimbai kama kuhudhuria
makongamano yakibiashara yanayo fanyika hapa nchini.
Aidha Mheshimiwa KADUMA amesema Taasisi ya Kingdom Leadrship Network
Tanzania imeandaa kongamano kubwa la kimataifa lijulikanalo kama Tanzania –
Israel Busines and Investment Forum(TIBIF) 2014 litakalo fanyika katika ukumbi
wa mwalimu nyerere jijinidar es salaam kongamano litakalo wakutanisa
watungasera,wataalamu,wenyeviwanda,wawekezaji na wajasiriamali wadogo,wakati na
wakubwa kutoka sektambalimbali hapa nchini.
Ameongeza kwamba lengo la
kongamano hilo nikuweza kuwawezesha wajasiriamali na wawekezaji kushirikiana
kibiashara,katika uwekezaji na kuibua furusa za uwekezaji kwa maendeleo ya
kiuchumi nakujifunza na kuchukua furusa ya maendeleo ya Israeli katika ubunifu
wa kisayansi na kiteknolojia kwa ajili ya maendeleo na kuimarisha ushirikiano
wa kimataifa na Israeli.
Kongamano hilo ambalo litafanyika
kuanzia tarehe 17/03/2014 limekusudia kutoa kipaumbele katika maeneo muhimu
kama Kilimo, Elimu, Afya na sekta mbalimbali kama
madini,ujenzi,viwanda,uhandisi,habari na mawsiliano,mali,utalii na kemikali.
Pia amewataka watanzania
kujitokeza zaidi katika kongamano hilo ili kuweza kijionea shughuli mbalimbali
zinazofanyika na wafanyabiashara maarufu,wajasiriamali wenye viwanda na kupata
kujifunza zaidi,.
Kwa wote wanao penda kushiriki
watumie mawasiliano ya simu +255 768 014 698, tovuti www.kingdomleadrship.net.tz au
barua pepe info@kingdomleadership.net.tz.
Charles Msamati
Hakuna maoni
Chapisha Maoni