Zinazobamba

mambo yanavyoendelea kampeni za ubunge Kenga




Meneja Kampeni wa Chama cha Deokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Alphonse Mawazo, akicheza ngoma ya jamii ya kimasai baada ya kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Grace Tendega Mvanda

Mzee wa Mila wa Kimasai katika Kijiji cha Mfyome, Lioper Ilmuduji, akimpatia baraka mgombea ubunge  wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Bi. Grace Tendega Mvanda, wakati chama hicho kilipofanya kampeni ya nyumba kwa nyuma kuomba kura kwa wananchi katika kijiji hicho.

. Mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Bi. Grace Tendega Mvanda akishiriki chakula cha kimila pamoja na watu wa jamii ya kimasai katika Kijiji cha Mfyome baada ya msafara wa mgombea huyo kufika kijijini hapo kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba.


Mgombea Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga, Grace Tendega Mvanda, akizungumza kuomba kura wakati chama hicho kilipofanya kampeni ya nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu katika Kijiji cha Mfyome.

Hakuna maoni