Diamond atupia swaga za Ngololo kwenye shughuli za mauli,
KIJOGOO wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
amewachefua waumini wenzake wa Kiislamu baada ya kutupia swaga za staili
ya Ngololo kwenye shughuli ya Maulidi.
Kijogoo wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz akicheza staili ya Ngololo kwenye kaswida.
Tukio hilo lililowagusa waumini hao lilitokea juzikati ambapo
kulifanyika Maulidi ya
kumtoa nje mtoto wa dansa wake aitwaye Moze
Lyobo maeneo ya Mbagala, jijini Dar.
Awali watu waliokuwepo eneo hilo walifurahia uwepo wake
lakini kadiri walivyoaanza kugundua kasoro ndipo mambo yalipoanza
kuharibika.
Diamond akiwa kwenye shughuli hiyo.
“Watu hawakumshtukia, lakini walipomkagua kwa makini na kugundua licha ya kuvaa mavazi ya
Kiislamu ndani yake ana macheni ya dhahabu shingoni kitu ambacho dini hairuhusu,” kilidai
chanzo baada ya mwandishi wetu kufika eneo la tukio na kukuta shughuli imeisha.
Kama hiyo haitoshi, ikaelezwa kuwa Diamond alizidi kuchafua hali ya hewa baada ya kucheza
staili ya Ngololo kwenye kaswida kitu ambacho kiliwashangaza wengi.
…Diamond akiwa na mtoto wa Moze Lyobo aliyefanyiwa Maulidi.
“Mwanzo alianza vizuri lakini kadiri dufu lilivyokuwa linakolea, akawa anajisahau na kucheza
Ngololo, kimsingi aliwaboa baadhi ya Waislamu waliokuwa pale,” alisema shuhuda wetu.
Hata hivyo paparazi wetu alitonywa kuwa, baada ya kucheza sana, Diamond alichoka huku jasho
likimchuruzika ambapo aliamua kupumzika na kuwaacha wengine wakiendelea.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni