Dkt. Kigoda: Fanyeni kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu mkubwa
Waziri
wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda( Katikati), Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Bw Uledi Mussa( Kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Bi Maria Bilia (Kulia), wakifuatilia mkutano wa Baraza la Wafanyakazi
wa Wizara hiyo unaofanyika JijiniDsm.Waziri
wa Viwanda na Biashara DktAbdallah Kigoda akitoa hotuba ya Ufunguzi wa
Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara yake unaofanyika JijiniDsm.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Wizaraya Viwanda na Biashara ambao ni wajumbe wa
Baraza la Wafanyakazi wanaoshiriki mkutano wao JijiniDsm
……………………………………
……………………………………..
Wafanyakazi
wa Wizara ya Viwanda na Biashara wametakiwa kuongeza juhudi na ubunifu
katika utendaji wa kazi ili kuiwezesha Wizara hiyo kufikia malengo yake
iliyojiwekea.
Wito
huo umetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.DktAbdallah Kigoda,
wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo
unaofanyika kwa siku mbili Jijini Dar Es Salaam.
Dkt.
Kigoda amesema, Wizara ya Viwanda na Biashara ina jukumu kubwa katika
kuboresha Uchumi wa Nchi hivyo wafanyakazi hawana budi kufanya kazi kwa
bidii na ubunifu ili kuiwezesha Wizara kupata matokeo yaliyokusudiwa.
“Fanyeni
kazi kwa bidii, kwa maarifa na ubunifu mkubwa. Epukeni uzembe,
ukiritimba usio na sababu za msingi na zaidi ya yote, tujitangaze ili
Umma ufahamu kikamilifu jitihada zetu katika kukuza uchumi’’.
Awali
akimkaribisha Mh Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw Uledi Mussa
amesema, Uongozi wa Wizara hiyo utaendelea kufanya jitihada za kuboresha
maslahi ya wafanyakazi, mazingira ya kufanyia kazi na kuondoa kero
mbalimbali zinazowakwaza watumishi.
Kwa
upande wake Mtoa mada katika Mkutano huo Bi Honesta Ngolly ambae ni
Afisa Elimu Kazi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi CMA, amewataka
watumishi na Viongozi wa Wizara kutimiza wajibu wao, kuheshimu sheria na
miongozo ya kazi ili kuepusha migogoro katika sehemu za kazi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni