Zinazobamba

MASHINE ZA EFDS BADO NI ZENGWE, WAFANYABIASHARA KARIAKOOO WAGOMEA SEMINA YA TRA, WASEMA HAINA FAIDA KWAO, WAWAOMBA TRA KUWA WASIKIVU

MENEJA WA KODI MKOA WA ILALA, KULIA AKIFUATILIA HOJA MBALIMBALI ZILIZOTOLEWA NA WADAU WA KODI KATIKA SEMINA YA NUSU SIKU ILIYOFANYIKA MAPEMA HII LEO JIJINI DARESALAM, KULIA KWAKE NI ndg.GEORGE HAULE AMBAYE NDIYE AFISA ANAYESHUGHULIKIA ELIMU KWA MLIPA KODI WILAYA YA ILALA

Wafanyabiashara wa soko la kariokoo ambapo hivi karribuni walileta tafrani kwa kuendesha mgomo wa kutofungua maduka yao wakidai kuwa gharama za mashine mpya zilizoingizwa na TRA kuwa juu kuliko nchi nyingine yeyote hapa duniani, leo wamegomea semina ya TRA wakisema semina za namna hiyo hazina tija kwao na badala yake wamewataka viongozi wa TRA kutafuta mbinu mbadala ya kuondoa changamoto zinazowakabili kwa sasa,

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mapema hii leo jiji Daresalaam, wafanyabiashara hao wamesema kwa sasa kilio chao kikubwa ni bei za mashine za EFDs ambazo ziko juu sana zaidi ya maelezo, lakini wanapozungumza na TRA wanaonekana kutojali hoja zao na badala yake wanaendelea na zoezi, kitu ambacho wameita ni ubabe uliopitiliza.
MMOJA WA WADAU AMBAYE AMEGUSWA NA TATIZO LA BEI YA MASHINE ZA EFDS AKIFAFANUA JAMBO KWA MAAFISA WA KODI, MKOA WA ILALA

Serikali hii ambayo inajinasibu kwa kuwa sikivu kwa wananchi wake hivi sasa ikichukua hatua za makusudi ya tatizo hili ambalo limeonekana kuwa ni onevu kwa wafanyabiashara wa hapa ndan
Wafanyabiashara hao wameenda mbele zaidi na kusema wafanyabiashara wa hapa nchini wameonyesha kukerwa kwao kwa bei za mashine hizi karibuni sehemu mbalimbali za kona ya nchi hii, kwanza ilikuwa kule Mbeya, wakarudi pale MOROGORO, ikaenda kule Lindi na hapa jijini Daresalaam ambapo katikati ya soko tuligoma kufungua maduka yetu ili tupate ufumbuzi

Wamesema haiwezekani mashine hizo hizo ambayo wafanyabiashara wa Bongo wanauziwa Ths 800000 nchi zingine duniani zinauzwa kwa dola 100, huo ni unyonyaji wa hali ya juu na kunauwezekano wa fedha hizo kutumika isivyo halali,
Hata hivyo semina hiyo iliendelea kama kawaida ingawaje wafanyabiashara hao hajahudhulia,

Alipoulizwa afisa wa elimu kwa mlipa kodi mkoa wa kikodi Ilala, Bw GEORGE HAULE amekiri kutokuwepo kwa wajumbe hao muhimu katika semina hiyo ya kuwapa elimu juu ya maashine hizo za EFDs lakini amesema hiyo haizui wao kuendelea kutoa elimu kwa wadau wengine kama wa TCIAA, wakuu wa shule ,wafanyabiashara wa spares ambao nao wanapaswa kupewa elimu stahili ya Mashine hizi za kodi
HAPA WAJUMBE WA KODI MKOA WA KIKODI ILALA  WAKIFUATILIA MAELEZO YA MTOA MADA KATIKA SEMINA HIYO YA KODI ILIYOFANYIKA MAPEMA HII LEO JIJINI DARESALAAM


MMILIKI WA SHULE ZA TUSIIME BW. ALBERT KATAGIRA AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA MAAFISA WA KODI MKOA WA ILALLA, KATAGIRA AMESEMA KUWA ELIMU KUHUSU UTOFAUTI KATI YA REPORT YA MAHESABU YA KIBIASHARA NA UTOAJI WA RISITI KWA NJIA YA MASHINE ZA KODI NI LAZIMA ITOLEWE KWANI WANANCHI WENGI WAMEKUWA WAKIOOGOPA KUNUNUA MASHINE HIZI WAKIDHANI KUWA MASHINE HIZO ZITAMUONYESHA TRA NAMNA KAMPUNI ILIVYOKUSANYA MAPATO YAKE YA NA MATUMIZI YAKE, KITU AMBACHO SIYO KWELI KWANI MASHINE HIZO ZINAONYESHA MAKUSANYO TU NA SIO MATUMIZI.




KATIBU WA WAFANYABIASHARA WA SPARE MKOA WA KIKODI ILALA A, BW. CYPRIAN ZAKARIA AKIFUATILIA KWA MAKINI MAELEZO YA MAOFISA WA KIKODI KATIKA SEMINA HIYO

TUKO MAKINI TUNAFUATILIA,

MUAKILISHI WA WADAU WA TCIAA AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WAJUMBE NA WADAU WA KODI MKOA WA ILALA, MJUMBE HUO AMEWATAKA MAMEJA WA KODI MKOA WA ILALA KUFANYA KAZI YA KABADILISHA MATAZO HASI  WA WAFANYABIASHARA WA KUTOPENDA KUTUMIA MASHINE HIZI NA WAANZE KUTUMIA MASHINE HIZI KWA WAKATI,

NACHANGIA,



No comments