AZAM TV YAANZA KUTOA HUDUMA ZAKE RASMI, WATEJA WAFURIKA, WASANII MBALIMBALI WAFUNGUKA.........
MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI YA AZAM MEDIA, AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI MAPEMA HII LEO KATIKA UZINDUZI RASMI WA AZAM TELEVISION KATIKA OFISI ZA TV HIYO JIJI DARESALAAM |
KEKI NZURI ILIYONAKISHIWA KWA MAJINA YA AZAM TV NAYO ILICHUKUWA UMUHIMU WAK KATIKA SIKU YA KUANZA RASMI HUDUMA YA AZAM TV, HAPA MKURUGENZI MKUU AKIWA WA KWANZA KURA KEKI HIYO, |
MONALISA NAYE HAKUWA NYUMA KUKAMATA FURSA, HAPA AKIPOZI KWA TABASAMU KATIKA SIKU HII AMBAYO AZAM TV INAZINDUA HUDUMA ZAKE RASMI KWA WANANCHI, LIGI YA VODACOM SASA LIVE NDANI YA KISIMBUZI CHA AZM TV |
MWENYEKITI NAYE ALIKUWEPO |
AzamTV leo imeanza kutoa huduma zake rasmi katika makao makuu yaliyopo
barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Huduma za matangazo ya AzamTV zilianza kupatikana hewani Kuanzia Ijumaa
Desemba 6, 2013 kwa kuwawezesha wateja waliounganishwa kwenya kisimbuzi
kungalia bure hadi hii leo ambapo huduma kwa malipo inaanza rasmi kwa ada
ya shilingi 12,500 kwa mwezi.
Kwa kuanzia huduma ya AzamTV itahusisha chaneli 50 zinazojumuisha chaneli
maarufu za kimataifa, chaneli maarufu za ndani na chaneli tatu maalumu za
Azam ambazo ni:
HIZI NDIZO HUDUMA
· Azam One – burudani kwa familia kutoka Afrika, sehemu kubwa ya
matangazo itakuwa kwa lugha ya Kiswahili.
· Azam Two – vipindi maalum kutoka sehemu mbalimbali za dunia
·SinemaZetu – Chaneli maalumu kwa tamthilia za kitanzania kwa saa
24.
AzamTV leo imeanza kutoa huduma zake rasmi katika makao makuu yaliyopo
barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Huduma za matangazo ya AzamTV zilianza kupatikana hewani Kuanzia Ijumaa
Desemba 6, 2013 kwa kuwawezesha wateja waliounganishwa kwenya kisimbuzi
kungalia bure hadi hii leo ambapo huduma kwa malipo inaanza rasmi kwa ada
ya shilingi 12,500 kwa mwezi.
Kwa kuanzia huduma ya AzamTV itahusisha chaneli 50 zinazojumuisha chaneli
maarufu za kimataifa, chaneli maarufu za ndani na chaneli tatu maalumu za
Azam ambazo ni:
· Azam One – burudani kwa familia kutoka Afrika, sehemu kubwa ya
matangazo itakuwa kwa lugha ya Kiswahili.
· Azam Two – vipindi maalum kutoka sehemu mbalimbali za dunia
· SinemaZetu – Chaneli maalumu kwa tamthilia za kitanzania kwa saa
24.
Kwa pamoja, chaneli tajwa zitawapa wateja wigo mpana wa kufaidi matangazo
bora ya michezo, tamthilia, watoto na maisha.
Ofisi ilifunguliwa rasmi na Bw. Yusuf Bakhresa: Mkurugenzi Mtendaji wa Azam
Media Ltd.
“Ofisi hii ya makao makuu ambayo kwa hakika ni ya kuvutia ni kielelezo cha
nia thabiti ya Azam Media kufanya kazi kwa umakini katika shughuli ya
utangazaji hapa Tanzania. Dira yetu ni kutoa burudani ya kiwango cha juu
kwa familia kwa bei nafuu kote nchini, na baadaye kote barani Afrika. Hili
ni jambo ambalo kila mmoja hapa nchini anapaswa kujivunia.” Alisema Bakhresa
Rhys Torrington: Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd alisema: “Naona
faraja kubwa kwamba leo hii AzamTV ipo sokoni kwa ajili ya kila mtanzania.
Tutahabarisha, kuelimisha na zaidi ya yote tutaburudusha watu kote nchini.
Huduma yetu inapatikana kwa watu wote – situ katika ofisi hizi lakini pia
kupitia mtandao wetu unaohusisha zaidi ya mawakala 50 katika kila mkoa.
AzamTV ni ya kudumu”
Azam Media pia inawekeza katika utayarishaji wa vipindi vipya kupitia
kampuni yake tanzu, Uhai Productions, kwa kushirikiana na watayarishaji wa
vipindi wa hapa Tanzania.
No comments
Post a Comment