Zinazobamba

WMA YAWAHIMIZA WANANCHI KUJIRIDHISHA NA VIPIMO KUTOKA KWA WAUZAJI WANAOWAPATIA HUDUMA.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa          umma(WMA)Veronica Simba

Na Mussa Augustine.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Wakala wa Vipimo Tanzania( WMA) Veronica Simba ametoa wito kwa Wananchi kutambua kuwa ni haki yao ya kuuliza na kujiridhisha kuhusu Vipimo vinavyotumika kuwapatia huduma kutoka kwa wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali zinazohusiana na Vipimo.

Rai hiyo ameitoa Julai 11,2025 Jijini Dar es salaam kwenye Maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba)nakubainisha kuwa Mwananchi yeyote anapokua na wasiwasi juu ya kipimo kinachotumiwa na muuzaji kumpa huduma,anapaswa kumuuliza muuzaji huyo ili kujiridhisha kama kimehakikiwa na Serikali kupitia Wakala wa Vipimo. 

"Kuuliza ni haki ya kila Mwananchi wala sio hisani kujiridhisha na kipimo chochote unapoenda kupata huduma,mfano umeenda duka la nyama( Bucha )umepimiwa nyama lakini una wasiwasi kama mzani huo umehakikiwa,una haki ya kumuuliza muuzaji akuonyeshe na ujiridhishe kwamba kuna stika ya Wakala wa Vipimo inayodhihirisha na kuthibitisha kwamba ule mzani umehakikiwa."amesema Bi.Simb
      Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa          umma(WMA)Veronica Simba

Nakuongeza"Tumegundua kwamba wapo wananchi wanaofahamu kuhusu Vipimo lakini bado wana uoga ,wanakosa ule uthubutu wa kuuliza,kwa mfano unaenda kupata huduma ambayo inahusiana na kipimo lakini unakuta Wananchi wengi wanakosa uthubutu wa kuuliza ili kujiridhisha kwamba kweli kipimo kilichotumika kumpatia huduma kimehakikiwa na Serikali kupitia Wakala wa Vipimo?"amesema.

Aidha ameendelea kubainisha  kuwa Wakala wa Vipimo umekuwepo kwenye maonyesho ya Sabasaba toka yalipoanza Juni 28 na mpaka sasa yanapoelekea ukingoni Juni 13 Mwaka huu,ambapo lengo lake la uwepo katika Maonyesho hayo limefikiwa kwa kiasi kikubwa kuliko hata walivyotarajia kwani wamepata fursa ya kuhudumia wananchi wengi ambao wamekua wakijifunza kuhusu Vipimo. 

"Kama mnavyofahamu sisi(WMA)jukumu letu kubwa ni kuhakiki Vipimo ili kumlinda mlaji wa bidhaa na huduma mbalimbali kutoka sekta tofauti zinazohusiana na vipimo,kuhakikisha mlaji anapata kilicho stahiki kulingana na vipimo."amesema

"Nakusisitiza kuwa"sisi(WMA)tupo katika sekta zote zinazohusiana na vipimo kuanzia sekta za Biashara ambapo kwenye biashara mfano maduka mbalimbali yanayouza bidhaa zilizofungashwa ikiweo maduka makubwa( Supermarkets)h bidhaa zote zinazouzwa Wakala wa Vipimo tunahakiki Vipimo vyake." 
    Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa          umma(WMA)Veronica Simba

Vilevile amesema kuwa"mfano unapoenda kununua bidhaa yoyote iliyopimwa kama vile kahawa,mafuta ya kupikia, Sukari au bidhaa yoyote unayokuta imepimwa na ikaandikwa kwamba kipimo kilichopo ndani unachokipata kipo kwa aina fulani labda kilo 2 au nusu kilo,robo lita, wewe unapoenda kununua unajuaje kwamba kweli kilichopo mle ndani ni sawa na kipimo kilichoandikwa pale juu? 

Kwahiyo hilo ni jukumu la Serikali kupitia Wakala wa Vipimo  kuhakikisha tunakagua ili wewe mnunuzi unapoenda kununua usipunjwe upate kile kilichoandikwa pale,hivyo  ni jukumu letu la kuhakiki Vipimo hivyo.
 
Ameendelea kufafanua kuwa kwenye sekta hiyo hiyo ya Biashara,mfano maduka ya Nyama(Bucha) kuna mizani zinazotumika,hivyo Wakala wa Vipimo unahakiki mizani hizo ili kuhakikisha kwamba ziko sahihi,nakwamba wanapomaliza uhakiki hua wanaweka stika(Lakiri)ambayo inasoma Wakala wa Vipimo ambayo inathibitisha kwamba ule mzani umehakikiwa. 

Aidha amesema Wakala huo  pia unahakiki Vipimo katika sekta nyingine kama vile Kilimo na Afya,ambapo kuna mizani ambazo zinatumika kupima mazao hususani ya kimkakati kama vile Korosho,Pamba,ili kumlinda mlaji na muuzaji ili pande zote mbili zipate kilicho stahiki.

Akizungumzia kwenye Sekta ya Afya Bi. Simba amesema Wakala huo upo kwa ajili ya kuhakiki Vipimo akitolea mfano mtu anapoenda hospitalini anapimwa uzito wake nakupewa  dawa kulingana na uzito,ambapo ni jukumu la Serikali kuhakiki Vipimo vile,nakusema kuwa Wakala huo unahakiki sekta zote zinazohusiana na vipimo ikiwemo Sekta ya Usafirishaji.

Katika haua nyingine amesema kuwa kuwa kutokana na mwitikio mkubwa wa Wananchi kujifunza kuhusu Vipimo Wakala huo umejengea taswira yakwamba elimu ya Vipimo niya msingi ,kwamba elimu hiyo inatakiwa isambae zaidi ili watu waipate kwa upana,ambapo WMA imekuja na mikakati ambayo inatamani kwenda kuitekeleza ili sasa ifikie sehemu kubwa zaidi ya jamii.

Ametaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuanzisha klabu mbalimbali mashuleni ili watoto waanze kujifunza kuhusu Vipimo,ambapo WRA itashirikiana na walimu kuanzisha klabu hizo ambazo zitakua niza mafunzo kwa ajili ya Sekta ya Vipimo kujua nini Serikali inafanya kupitia Wakala wa Vipimo.
Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Temeke Hilolimus Mahundi.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Temeke Hilolimus Mahundi amewashauri Wananchi wanapoenda kununua Nishati ya gesi ya kupikia  wahakikishe ile gesi wanapimiwa kwenye mzani ambao umehakikiwa na Wakala wa Vipimo. 

"Mwananchi unapoenda kuchukua gesi ya kupikia hakikisha kwanza unasoma maelekezo ya mtungi yameandikwaje,na kabla hujauchukua kwenda nao nyumbani hakikisha umeupima kama kweli upo sahihi,na ukiona haupo sahihi sisi WMA tuna Ofisi kila Mkoa unaweza kutoa taarifa ili upate msaada wa kisheria"amesema Mahundi. 

No comments