HAWA NDIO WALIOFUTWA KAZI NA JK, NI BAADA YA KAZI NZURI YA BUNGE
![]() |
RAIS WA TANZANIA MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PICHA NA MAKTABA YETU |
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki ametangaza Bungeni
kuwa amejiuzulu kutoka katika wadhifa wake huo kutokana na Ripoti ya
Kamati iliyoundwa kuchunguza madhila yaliyotokana na Operesheni Tokomeza
Ujangili, operesheni iliyotekelezwa na Wizara yake ikishirikiana wa
Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kagasheki alitoa kauli yake hiyo na kusema kuwa anapaswa kuwajibika,
mara tu alipozungumza baada ya wabunge kuchangia hoja hiyo iliyotikisa
Bunge na kuleta simanzi kubwa kutokana na unyama uliofanywa dhidi ya
wananchi ikiwemo kuteswa, kubakwa kwa wanawake na wengine kuuawa, adha
iliyoikumba pia mifugo. , Kagasheki alisema anapaswa kuwajibika.
Taarifa zaidi za Bungeni zimesema kuwa Rais Kikwete amepokea ripoti
husika na kuridhia kuwafuta nafasi za uwaziri mawaziri wanne.
Uamuzi huo ambao umesomwa na Waziri Mkuu, Mizengo PInda umewataja
mawaziri waliofutwa kazi kuwa ni Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani),
Shamsi Vua Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Mathayo David
Mathayo (MIfugo na Uvuvi) na Hamisi Kagasheki (Mali asil na Utalii).
No comments
Post a Comment