UKWELI ULIOJIFICHA KUHUSU KUVULIWA UONGOZI BW. ZITO KABWE, HALI YA KISIASA NDANI YA CHADEMA SI SHWARI..
Na Karoli Vinsent
Hali ya kisiasa ndani ya chama cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema imefikia pabaya baada ya kumvua uwongozi wa juu Zitto Kabwe.
Zitto ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini,ikumbukwe mwanzoni
mwa Novemba mwaka huu aliingia katika malumbano na Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema kuhusiana na masuala ya posho, akituhumiwa na Lema kuwa anakataa
posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho kutoka mashirika mbalimbali
Dar es Salaam. Suala
la hatma ya Naibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto
Kabwe ndilo lililotawala katika siku ya pili ya kikao cha Kamati Kuu ya chama
hicho na kusababisha mvutano mkali miongoni mwa wajumbe.Pamoja na ukweli kuwa kulikuwa na ajenda kadhaa zilizokuwa zimepangwa kujadiliwa katika kikao hicho cha siku mbili kilichofanyika Dar es Salaam, suala la Zitto ndilo lililochukua muda mrefu zaidi kujadiliwa.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho ambayo imeifikia habari24 kuwa kikao hicho zilieleza kuwa wajumbe waligawanyika makundi mawili, baadhi wakipendekeza Zitto avuliwe nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu kwa maelezo kuwa anakwenda kinyume na taratibu za chama hicho na wengine wakipinga hatua hiyo kwa maelezo kuwa haina tija.
Mpaka saa moja usiku jana jioni ambapo habari 24 ilizipata ni kuwa kikao hicho kilikuwa bado kikiendelea na suala hilo lililokuwa chini ya ajenda ya hali ya siasa nchini.
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi wa chama hicho, Benson Kigaila aliahidi kuwa taarifa rasmi ya kikao hicho ingetolewa baadaye na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Tuhuma za Zitto
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, mwanzoni mwa Novemba mwaka huu aliingia katika malumbano na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuhusiana na masuala ya posho, akituhumiwa na Lema kuwa anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho kutoka mashirika mbalimbali nchini.
Pia, aliingia katika malumbano na chama chake baada ya kutumia kofia yake ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Kauli ambayo jana Kigaila aliitolea ufafanuzi na kueleza kuwa Chadema kimekaguliwa na hesabu zake tayari zipo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Hekaheka za jana
Mvutano wa jana ulianza baada ya Mbowe kufungua kikao hicho saa 4:00 asubuhi.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilizoifika habari 24 zilieleza kuwa baadhi ya wajumbe, wakiwamo wabunge, walitaka Zitto avuliwe nafasi aliyonayo na kuwa mwanachama wa kawaida, huku wengine wakipinga hatua hiyo kwa maelezo kuwa Zitto hakuwepo katika kikao hicho na kwamba alipaswa kusikilizwa.
“Baada ya hali kuwa hivyo, Mbowe alipendekeza kuwa Zitto asijadiliwe kwa kuwa hakuwepo katika kikao hicho,” kilieleza chanzo cha habari hizo.
Zitto alikuwa katika safari ya kikazi huko Sudan Kusini akiwa amefuatana na wajumbe wa PAC.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Zitto alitafutwa na alituma salamu kwa wajumbe wa kikao hicho akiwaeleza kuwa alikuwa njiani na kuahidi kuwa angehudhuria mara tu baada ya kuwasili.
“Zitto alituma ujumbe kuwa anakuja katika kikao, kilikuwa na ajenda nyingi lakini suala lake lilijadiliwa kwa kirefu sana,” kilieleza chanzo chetu. Licha ya ombi la Mbowe, bado wajumbe walishinikiza kuendelea kumjadili Zitto hivyo ni kusababisha kuchelewa kujadiliwa kwa ajenda nyingine.
Tangu juzi, siku ya kwanza ya kikao hicho, ulinzi uliimarishwa nje ya Jengo la Ubungo Plaza na jana walinzi wa chama hicho, Red Brigade waliwatimua waandishi wa habari waliokaribia eneo hilo wakisema hayo ni maagizo kutoka kwa uongozi wa juu.
Yaliyojadiliwa
Katika ufafanuzi wake kwa waandishi wa habari jana jioni, Kigaila alisema kikao hicho kilichoanza juzi, kimejadili mambo mbalimbali. Alisema juzi kikao hicho kilijadili muhtasari wa vikao viwili vya dharura vya Kamati Kuu vilivyofanyika hivi karibuni.
“Tumejadili taarifa ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki, Zanzibar unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni... tunathibitisha kuwa tutashiriki,” alisema.
“Kulikuwa na taarifa ya hesabu za chama zilizokaguliwa na kupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na taarifa za fedha za utendaji kuanzia Kamati Kuu iliyopita mpaka Kamati Kuu ya sasa,” alisema Kigaila.
Huku akionyesha kitabu cha ukaguzi wa fedha mwaka 2010/11 na 2011/12 alisema: “Kamati Kuu imeridhika kuwa chama kimekaguliwa na hatuna deni kwa msajili.
Ajenda za jana
Alisema kikao cha jana kilijadili ajenda za uboreshaji wa jengo la makao mkuu pamoja na kupanga upya kurugenzi za chama hicho pamoja na nguvu kazi ya makao makuu ili kuweza kutekeleza vizuri majukumu yake.
“Ajenda inayoendelea hivi sasa ni ya uundaji wa programu ya `Chadema ni Msingi’, ambayo lengo lake ni kukijenga chama katika ngazi za chini kabisa. Huu ni mpango mkuu wa chama wa `Vuguvugu la Mabadiliko’ (M4C). Ajenda ya mwisho itakuwa ni kujadili hali ya kisiasa nchini.”
Zitto atinga usiku
Zitto alifika katika kikao hicho jana saa 2.24 usiku akiwa na walinzi wanne na habari kutoka ndani zinasema kwamba mara baada ya kuingia, ajenda ya kumjadili ilirejea. Ilielezwa kwamba alipewa nafasi ya kujitetea baada ya kusomewa ‘mashtaka’ yaliyokuwa yakimkabili.
Mwandishi wa blog hii aliyekuwa katika eneo hilo anasema baada ya kurejeshwa kwa agenda hiyo malumbano makali yalizuka kwani wajumbe walikuwa wazungumza kwa sauti za juu na jazba kiasi
Huku wakikosa imani na Zitto
Kabwe kwa kitendo chake cha kukisariti
chama hicho,kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kilichopo ndani ya mkutano
huo jana kilisema ajenda ya kumfukuza Zitto Kabwe jana ilikuwa ukitawala na
kufikia hatu ya kifika hatua ya kumvua uongozi wa chama hicho na pia na kutaka
apewe siku kazaa kwann asivuliwe uwana chama wa chama hicho.
Uchunguzi uliofanywa na
Habari24 umebaini, uwenda yale yalioandikwa kwenye wakala uliosambazwa kwenye
mitandao juu ya hujuma anayofanya zitto
kabwe na kushikiliana na baadhi ya maofisa wa usalama wa taifa kuhusu kukiujumu
chama hicho uwenda ikawa sababu iliyowafanya baadhi ya wajumbe wa mkuto huo
kumfukuza zitto kabwe,
Ikumbukwe baada ya kusambaa
kwa walaka huo kwenye mitandao ya kijamii wenye kichwa cha habari walaka wa
siri kuhusu Zitto kabwe,Zitto kabwe mwenyewe aliibuka na kuupinga walaka huo na
baadhi ya viongozi wa chadema pia waliupinga walaka huo wakisema huwenda ni
ujuma za baadhi ya watu wasiokitakia jema chama hicho.
Katika hari ya kushangaza
mwandishi wa blogs alishuhudia kwenye mitandao wa kijamii amabapo uliwekwa
walaka huo, katika hali ya kushangaza baadhi viongozi wa chama cha chadema waaliweka
alama ya ku like kama kuunga mkono yale yalioandikwa kwenye walaka ule na pia
jambo jingine walaka ule ulichapishwa kwenye
blog ya kiongozi wa chadema na jina tunalo tunaliifadhi na kutia mashaka
kuhusu ukweli walaka huo
Habari hii imeandikwa na
Karoli vinsent pamoja na kushirikiana na Gazeti la mwananchi pamoja na vyanzo
mbalimbali ndani ya chadema
Hakuna maoni
Chapisha Maoni