OASIS YARIDHISHWA NA MFUMO WA KIDIGITALI WA TRA KUHUSU KODI.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya OASIS Financial Services Ltd.,Bw.Stambuli.Myovela
Na Mussa Augustine.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya OASIS Financial Services Ltd inayojihusisha na masuala ya ushauri wa kodi,Bw.Stambuli Myovela amesema kuwa mifumo ya kisasa ya kidigitali ya ukusanyaji wa kodi iliyoanzishwa na Mamlaka ya Mapato Nchini(TRA)itasaidia kuvutia wawekezaji wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi.Myovela amesema hayo leo Machi 23,2026 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya mafunzo yaliyoandaliwa na TRA kwa kushirikiana na jumuiya ya wafanyabiashara wa kichina,pamoja na kampuni ya OASIS Financial Services Ltd.,
nakuhudhuriwa na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) Yusuph Mwenda pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania,ambapo Viongozi hao kwa pamoja wameonesha nia ya kutatua mambo yanayohusu kodi katika jumuiya za wafanyabiashara nchini humo.
"TRA imekua ikifanya Mapinduzi yakimfumo kutoka ile mifumo ya kizamani kuja mfumo wa kisasa wa kidigitali ambao unaweza kulipa kodi na ukawa unawasiliana na TRA sehemu yoyote duniani,kitendo cha kwenda kwenye ofisi za TRA mfumo huu umepunguza kwa kiasi kikubwa,
kwasababu kuanzia usajiri,kuwasilisha ritania,kupata cheti cha kodi(tax clearance certificate)kufanya mapingamizi ya kodi,makadirio na mazungumzo ya kinyaraka yanafanyika kupitia mfumo wa kidigitali."amesema
Amesema kuwa mfumo huo unawezesha kodi kua za uhakika na kuaminika,nakwamba mfumo huo umeunganishwa na mifumo mingi ya Serikali hivyo makadirio ya kodi yanakua zaidi ya uhalisia kuliko yale ya kukadiria.
Aidha Myovela ameendelea kusisitiza kuwa mazingira ya Tanzania bado ni mazuri kwa uwekezaji kutokana na kuwepo kwa rasilimali nyingi na jiografia nzuri,ustahimilivu wa kisiasa,Mapinduzi ya kimfumo,kuliko nchi nyingine za afrika mashariki.
Katika hatua nyingine Bw.Myovela amesema kuwa upande wa china kati ya miradi iliyosajiliwa mwaka 2023/2024 na kituo cha uwekezaji Tanzania(TIC),ilikua na thamani ya dola billion 1.7 ambazo ni sawa na zaidi ya Tsh. trioni 4.
"Kati ya miradi hiyo wawekezaji wa kichina waliwekeza Dola bilioni 1.053,ni sawa na asilimia 60 ya zaidi ya trioni 4 zilizotokana na uwekezaji wa wafanyabiashara wa jumuiya ya china( foreign direct investment)hali ambayo imeonesha namna wafanyabiashara wa kichina walivyoweza kuleta mitaji yao na kufungua biashara na makampuni."amesema.
Nakuongeza kuwa "kwa sasa bidhaa nyingi hapa Nchini zinazalishwa na wa china,akitolea mfano vigae( tyles),vioo,sabuni za unga,vipuli,uunganishaji wa magari mapya,hatua ambayo inasaidia pia Watanzania kujifunza uwekezaji Viwanda pamoja na Teknolojia.
"Muamko wa Watanzania kufungua viwanda umekua mkubwa,saivi kuna viwanda vingi vinamilikiwa na Watanzania,hii inamaanisha kuwa hawa wenzetu wameleta Mapinduzi makubwa ya Teknolojia (technological transfer)kupitia mashine,ujuzi nakufungua ajira na soko kwa pande zote mbili za Tanzania na China."







No comments
Post a Comment