RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ALISHIRIKI SALA YA EID-AL FITR KATIKA MSIKITI WA MSOGA.
Na Mwandishi Wetu.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 21 Machi 2026 alishiriki sala ya Eid al-Fitr katika Msikiti wa Msoga uliopo mkoani Pwani.
Akizungumza mara baada ya ibada hiyo, Dkt. Kikwete alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani, mshikamano na umoja miongoni mwa Watanzania. Alieleza kuwa mafanikio ya taifa yanategemea zaidi utulivu na ushirikiano wa wananchi wake, akiwataka Watanzania kuendelea kuheshimiana bila kujali tofauti zao za kidini, kikabila au kisiasa.
Aidha, aliwataka waumini kutumia mafunzo ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kama chachu ya kuendeleza matendo mema katika maisha ya kila siku, ikiwa ni pamoja na kusaidiana na kujali wenye uhitaji katika jamii.
Sherehe za Eid El Fitr huadhimishwa na Waislamu duniani kote kama ishara ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi wa Ramadhani, zikiambatana na sala, furaha na matendo ya huruma kwa jami



No comments
Post a Comment