Zinazobamba

VIJANA WATAKIWA KUWA WAZALENDO KUWAENZI VIONGOZI WALIOKOMBOA BARA LA AFRIKA.


Na Mussa Augustine.

Vijana wa kitanzania wamesisitizwa  kulinda amaAni pamoja nakua Wazalendo katika Taifa lao ili kuweza kuwaenzi Viongozi waliopigania uhuru kwa ajili ya ukombozi wa nchi za bara la Aftika.

Wito huo umetolewa leo Machi,23,2026 jijini Dar es salaam na Mkurugenzi msaidizi urithi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  Dkt.Julieth Kabyemela wakati akifungua mdahalo unaohusu maadhimisho ya siku ya ukombozi wa nchi za kisini mwa Afrika uliyofanyika katika kituo cha  urithi wa ukombozi wa  afrika.

"Watanzania ni muhimu sana katika kutoa elimu kwa jamii,hususan kwa vijana,ili waweze kufahamu ukubwa wa nchi yao na historia yake adhimu,ili pia waweze kua Wazalendo kwenye Taifa lao"amesema Dkt.Kabyemela.Aidha amesema kuwa Tanzania ina urithi wa kipekee ambao hautofautiani tu,bali pia una thamani kubwa ukilinganisha na nchi nyingine nyingi barani Afrika.

Aidha ameongeza kuwa kwa msingi huo,siku hiyo ya maadhimisho ya siku ya ukombozi wa nchi za kisini mwa Aftika inayofanyika Machi 23 kila mwaka chini ya SADC ina umuhimu mkubwa kwa watanzania  kama taifa,na huadhimishwa kwa namna mbalimbali ili kuendeleza uelewa huo. Kwa upande wake Mratibu wa Kituo Cha urithi wa Ukombozi wa Aftika Bw.Christopher  Mhongole amesema kuwa kituo cha urithi wa ukombozi wa Afrika kimeandaa matukio maalum,ikiwemo onyesho la kihistoria pamoja na mdahalo unaowakutanisha wadau mbalimbali kujadili kwa kina masuala ya historia na ukombozi wa bara la Afrika.

Aidha amesema lengo kuu ni kutoa elimu kwa jamii ili iweze kufahamu historia yao, kutambua urithi uliopo nchini kama ushahidi wa historia hiyo,na kushiriki kikamilifu katika juhudi za kuhifadhi na kuuenzi urithi wa ukombozi wa Afrika.

"Kupitia historia hii,wananchi hususani vijana wanapata fursa ya kujifunza uzalendo kutoka kwa viongozi waliopigania uhuru na maendeleo ya Afrika, na hivyo kuhamasika kuendeleza juhudi hizo kwa manufaa ya taifa."amesema Bw.Mhongole

Nakuongeza kuwa "Kituo hiki pia kina jukumu la kuimarisha ushirikiano miongoni mwa nchi za Afrika,ni kituo kilichoanzishwa kwa azimio maalum la Umoja wa Afrika mwaka 2011, kikilenga kuratibu, kuhifadhi na kusukuma mbele juhudi za uhifadhi wa historia na ushirimi arithi wa bara zima."

Bw.Mhongole amesema kuwa kupitia mchango wa Tanzania katika ajenda hii,nchi imepewa heshima ya kuwa kitovu cha taarifa muhni imu za kihistoria kwa bara la Afrika.r

Ameongza kuwa mataifa mbalimbali yanatambua kuwa Tanzania ni mahali sahihi pa kupata kumbukumbu na maarifa kuhusu historia ya ukombozi na urithi wa Afrika kwa ujumla.Hata hivyo baadhi ya washiriki wa mdahalo huo akiwemo Jesca Monahera mwanafunzibwa kidato cha 6 kutoka shule ya Sekondari Zanaki,na Mwenyekit wa taasisi ya Eagle Coy Foundation(ECF) Lugano Daud wamesema kuwa jamii hususani vijana wanapaswa kujifunza ili waweze kujua namna uhuru ulivyopatikana pia kuendelea kuwa Wazalendo,na kuwaenzi Viongozi wa Afrika waliopigania uhuru barani inAfrima.

No comments