SEKTA YA VIWANDA IMECHANGIA ASILIMIA 7.3 PATO LA TAIFA.
Imeelezwa kuwa mwaka 2024,sekta ya viwanda ilichangia asilimia 7.3 ya pato la Taifa,ikilinganishwa na asilimia 7.0 mwaka 2023.
Vilevile,ukuaji wa sekta hiyo uliongezeka kutoka asilimia 4.3 mwaka 2023 hadi asilimia 4.8 mwaka 2024,ikiashiria kuwepo kwa uimara wa sekta.
Hayo yamebaishwa leo Desemba 18,Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelezea,mafanikio na mipango mikakati ya Wizara hiyo katika kuinua sekta ya Viwanda na biashara katika Serikali ya awamu ya sita.
Aidha amesema kwa upande wa sekta ya biashara,mchango wake katika pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 8.4 mwaka 2023 hadi asilimia 8.6 mwaka 2024, huku kasi ya ukuaji ikipanda hadi asilimia 4.8.
Amesema kuwa ongezeko hilo limetokana na maboresho makubwa kwenye mazingira ya biashara,upanuzi wa viwanda vinavyoongeza lakini pia na juhudi za Serikali kufungua masoko mapya ya kikanda na kimataifa.
"Thamani ya bidhaa zilizozalishwa viwandani ilifikia Sh. 26,438.5 bilioni mwaka 2023, ikiongezeka kutoka Sh. 25,034.5 bilioni mwaka 2022, sawa na ongezeko la 5.6% katika thamani ya uzalishaji."amesema Waziri Kapinga.
Nakuongeza kuwa "Tunapozalisha bidhaa tunategemea kuuza ndani na nje ya nchi,tunahitaji masoko ya uhakika,tunayo masoko ya kikanda ambayo yameleta tija kubwa katika biashara".

No comments
Post a Comment