MCH.MWIZAGI AISIHI JAMII KULINDA AMANI NA UMOJA WA KITAIFA.
Na Mussa Augustine. Kitunda,Dar es salaam.
Mch.Mwizagi amesema hayo Desemba 15,2025 wakati akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake kuelekea maadhimisho ya sherehe za sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya,nakubainisha kwamba jamii hususani Vijana wasitumie vibaya mitandao ya kijamii kwa kuhamasisha chuki na vurugu zinazopelekea uvunjifu wa Amani.
Aidha amesema kuwa kwa sasa mmomonyoko wa maadili umekua mkubwa katika Jamii kutokana na kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya teknolojia Duniani.
"Sikukuu ya krismas inatukumbusha kuzaliwa kwa mwokozi wetu Yesu Kristo,hivyo tunaposheherekea siku hii muhimu lazima tukumbushane kulinda amani na umoja wetu wa Kitaifa ambapo ni jambo muhimu sana kwa Taifa letu" amesema Mch..Mwizagi
Aidha Kiongozi huyo wa Kiroho pia amesema kuwa Vijana wengi maarufu kama Gen-z wamekuwa wakijihusisha kwenye vitendo vya vurugu kutokana na kukosa hofu ya Mungu mioyoni mwao.
"Tunamaliza mwaka 2025 tunaingia 2026 tunapaswa kuendelea kupendana na kukaribishana ili tusherehekee pamoja kwa upendo siku ya mwaka mpya,tuwe watulivu na tujilinde na mambo yasiyofaa" amesisitiza Mch.Mwizagi.
No comments
Post a Comment