Zinazobamba

TANFORD KUWAKUTANISHA WADAU WA BIASHARA,UWEKEZAJI,USAFIRISHAJI NA UCHUMI KUTOKA TANZANIA.

Na Mussa Augustine.

Kampuni ya TANFORD Businessmen Administrative Services L.L.C iliyopo Dubai imeandaa Kongamano la Kimataifa(Tanzania Trade and Logistics Forum 2026)litakalowakutanisha wadau muhimu wa biashara,uwekezaji, usafirishaji na uchumi kutoka Tanzania, United Arab Emirates(UAE),Afrika Mashariki,GCC na nchi zisizo na Bandari( Land Locked Countries).

Akizungumzia na Waandishi wa habari leo Desemba 16,Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw.Hussein Jamali amesema kuwa Kongamano hilo litafanyika Februari 13 na 14,2026 Dubai UAE ikiwa lengo ni kukuza biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na United Arab Emirates(UAE) pamoja na GCC katika kuleta wawekezaji wakubwa,taasisi za kifedha,makampuni ya masoko na wazalishaji ili kujua fursa zilizopo nchini Tanzania.

Aidha amesema kuwa Kongamano hilo pia litachagiza kutangaza fursa zilizopo Tanzania,ikiwa ni pamoja na Mamkala ya Bandari Nchini(TPA),Shirika la Reli Nchini( TRC),Mamlaka ya Anga(TAA),Mamlaka ya maendeleo ya Biashara Nchini(TANTRADE),Mamlaka ya uwekezaji na maeneo maalumu ya kiuchumi(TISEZA),Mamlaka ya kukuza uwekezaji Zanzibar(ZIPA),na Taasisi zingine za Serikali na Biashara.

Ametaja malengo mengine ya Kongamano hilo kuwa ni pamoja na kujenga majukwaa ya ushirikiano kati ya Sekta binafsi na Serikali kwa ajili ya mikataba,ubia na ujenzi wa miradi ya kimkakati,kuunga mkono makampuni ya Cargo,Clearing & Forwarding na Logistics kwa kuyakutanisha na masoko mapya ya UAE,GCC na Asia. 

Aidha ameendelelea kufafanua kuwa Kongamano hilo pia litapanua fursa kwa Vijana kupitia program ya Youth Innovation and Business Stage ambapo Vijana wenye mawazo ya biashara watapata nafasi ya kuwasilisha miradi yao mbele ya wawekezaji,na kuongeza uwekezaji wa moja kwa moja(FDI) kutoka UAE kwenda Tanzania.

"Pamoja na malengo hayo lakini Kongamano hilo pia litasaidia makampuni ya Tanzania kupenya katika soko la Kimataifa,kujenga mitandao ya biashara yenye tija,kufungua milango ya ushirikiano kwa nchi zisizo na Bandari zinazotumia Tanzania kama lango la biashara,kuboresha taswira ya Tanzania kama kitovu cha biashara,utalii na uchumi wa Viwanda" amesema Bw.Jamali.

Aidha amebainisha kuwa washiriki wa Kongamano hilo ni pamoja na Taasisi za Serikali na Makampuni ya Sekta binafsi kutoka Tanzania na UAE ,GCC,Asia na Afrika,Taasisi za kifedha,wawekezaji wakubwa na wawekezaji binafsi(Angel Investors & Venture Capital),Nchi zisizo na Bandari,wadau wa Cargo,Logistics, Shipping and Supply chain,pamoja na Vijana wa Tanzania kupitia Youth Innovation & Business Stage. 

"Mada kuu zitakazojadiliwa kwenye Kongamano hilo ni pamoja na biashara na masoko ya Kimataifa,Logistics,Cargo & Supply chain,Teknolojia na Digital trade,uwekezaji katika viwanda na kilimo,Bandari,Reli,Anga na biashara, Financing Trade na Export,Youth Innovation and Startups Pitching" amesema Bw. Jamali 

Nakuongeza "Tunatarajia baada ya Kongamano hilo mikataba ya biashara kati ya Makampuni ya Tanzania na United Arab Emirates(UAE),ushirikiano wa Taasisi za serikali,kuongzeka kwa Visibility ya Tanzania Kimataifa, kupanuka kwa masoko ya bidhaa na huduma za Tanzania,kuimarika kwa mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na UAE pamoja na Vijana kupata mitaji na ushauri kwa miradi yao. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TATOA Elias Lukumay amewataka vijana kuchangamkia fursa hiyo ili kukuza biashara zao na kuongeza ufanisi.

Naye Rais wa Chama Cha Mawakala wa forodha Nchini(TAFA) Edward Urio amesema kongamano hilo lina umuhimu mkubwa katika sekta ya usafirishani wa mizigo nani fursa kwa nchi zisizo na bandari na zinazotumia bandari ya Dar es Salaam.

Kampuni ya TANFORD Businessmen Administrative Services ni kampuni yenye makao yake makuu Dubai-UAE ambayo imeundwa na Watanzania wanaofanya kazi katika sekta ya Logistics,Cargo,na biashara katika United Arab Emirates. 

No comments