HATUWEZI KUUZA UHURU WETU KWA WAZUNGU:MCHANGE

Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali za Taifa (MECIRA) Habibu Mchange, amekemea kauli za baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaodaiwa kutaka kuirudisha Tanzania katika mifumo ya kikoloni au ya kitumwa
Ametoa kauli hiyo leo, Desemba 12, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akijibu hoja za Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA John Heche kufuatia tamko lililotolewa na chama hicho.
Mchange amesema MECIRA kama sehemu ya Watanzania wanawakumbusha wanasiasa wote kuwa maslahi ya Taifa ni muhimu zaidi kuliko maslahi ya vyama vyao.
No comments
Post a Comment