VETA YAUNGA MKONO AGENDA YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI KWA VITENDO.
Na Mussa Augustine.
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA)inatengeneza majiko ambayo yanatumika kwa ajili ya Nishati Safi ya kupikia kwenye maeneo ya watu wengi ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Ris wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,kwamba ifikapo mwaka 2034 zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanatumia Nishati safi ya Kupikia.
Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 7,2025 na Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore wakati alipotembelea banda la VETA katika Maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es salaam.
"Kwa sasa tunaongelea suala la Nishati safi ya kupikia,ambapo Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekua ni kinara katika kuhakikisha kwamba Nchi inatumia Nishati safi ya kupikia."amesema
Nakuongeza"Sisi kama VETA tumekuja na eneo la utengenezaji wa majiko ambayo yanatumika kwenye maeneo yale makubwa ya kutumia watu wengi,Serikali ilielekeza Taasisi,na Mashirika ya Serikali na Binafsi yenye kulisha zaidi ya watu 100,kutoka kwenye matumizi ya mkaa nakuhamia kwenye matumizi ya Nishati safi."
Aidha amesema kuwa ili kuweza kufanikiwa agenda hiyo ya serikali ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia lazima kuwepo na vifaa vinavyohitajika kuwepo,nakwamba VETA inatengeneza majiko yakuweza kutumika katika maeneo hayo.
"Kwahiyo tunawakaribisha kwa ajili ya kupata majiko lakini pia kuhakikisha kwamba ile sera na ile jitihada ambayo mhe. Rais amekua aki iishi katika matumizi ya Nishati safi na sisi tunaitekeleza nakuhakikisha wananchi wanatambua na wanakua na uwezo wa matumizi ya Nishati hiyo.
Nakuongeza kuwa "Sambamba na hilo tunawakaribisha wananchi waje kwenye banda letu kuja kuaona vitu ambavyo VETA tunavifanya,tuna mageuzi makubwa sana,tumeyafanya katika Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi hapa Nchini,na sasa hivi tunatoa ujuzi mwingi sana,kila eneo la ujuzi tunalo,hakuna eneo ambalo wewe utakuja utasema hujui."
Halikadhalika amesema kwa sasa VETA pia inatoa ujuzi wa wale watu wanaofanya kazi majumbani nakuweza kuhudumia wazee,nakwamba wanalo darasa ambalo wamehitimu karibu watu 700 na wapo kwenye ajira.
"Tunapenda kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuweka msisitizo katika hii Elimu ya Amali(Ufundi stadi),ambao sisi kwetu VETA tumeona manufaa makubwa sana,na tumefaidika sana,na Rais ameweza kutekeleza mambo mengi sana,kwasasa tuna vyuo vya Veta 80 Nchini vinavyofanya kazi,na vipo vyuo 65 ambavyo Serikali inaenda kuvimalizia."amesema
Aidha amesema kuwa Rais Dkt.Samia ametoa takribani bilioni.100 kwa ajili ya ujenzi huo na ujenzi upo katika hatua nzuri katika ukamilishaji wa awamu ya kwanza,hivyo VETA itakua na jumla ya vyuo 145 hapa nchini,ambapo kila Wilaya hapa nchini itakua na chuo Cha Ufundi Stadi.
Amehitimisha kwa kuongeza kuwa Vyuo hivyo vinaenda kusaidia wananchi kuweza kupata urahisi wa elimu na ujuzi ambao wanauhitaji,lakini pia lengo la vyuo hivyo ni kuhakikisha mafunzo yanatolewa kulingana na shughuli za kiuchumi na shughuli za kijamii zinazo fanyika katika kila Wilaya.
No comments
Post a Comment