BODI YA TFRA YAIOMBA KAMPUNI YA AGRAMI AFRIKA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA KWA WAKULIMA
Na Mwandishi Wetu. Dar es salaam.
Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imetoa rai kwa kampuni ya Agrami Afrika kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima wanaowahudumia Ili wazalishe kwa tija.
Rai hiyo imetolewa na mjumbe wa bodi hiyo Dkt. Shimo Peter, alipotembelea banda la kampuni ya Agrami Afrika na Mzuri Afrika katika maonesho ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam (DITF) maarufu Sabasaba.
Dkt. Shimo amesema kuwa ni jukumu la pamoja la wadau na wafanyabiashara wa Mbolea kuhakikisha wanatoa huduma iliyokamilika kwa kuuza na kutoa elimu ya kuzitumia mbolea hizo Ili zilete matokeo mazuri shambani." Nyinyi mmesajiliwa na TFRA mnaingiza mbolea zenu na kuwauzia wakulima, sasa hakikisheni mnawaelimisha wakulima wenu kanuni za matumizi sahihi ya mbolea ili wapate matokeo mazuri kwamaana ya kuzalisha kwa tija, alisema Dkt. Shimo.
Ameongeza kuwa kwa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima wanaowahudumia itaongeza thamani ya huduma wanayotoa na kukuza biashara ya mbolea zao, tofauti na kuuza bila kuelimisha matumizi.
Kwa upande wake Afisa kilimo wa kampuni hizo Salim Msuya amesema kuwa mara zote wanatoa huduma zaidi ya moja kwamaana ya kuuza mbolea zao, kutoa elimu na ushauri ili kumuwezesha mkulima anaetumia mbolea za Agrami kupata matokeo mazuri yaliyotarajiwa.
Msuya akafafanua kuwa utaratibu wa Agrami Afrika na Mzuri Afrika ni kukusanya taarifa za wakulima wanaowahudumia na kuwafanya wanafamilia jambo linaongeza ufanisi na urahisi wa utoaji huduma, kwakufuatilia maendeleo ya shamba la mkulima husika kwa kupiga simu na kumtembelea shambani kujiridhisha maendeleo ya mazao shambani."Asante kwa ushauri mkuu naomba nikutoe wasiwasi, sisi Agrami Afrika na Mzuri Afrika mteja kwetu ni mwanafamilia, tunashirikiana ne hatua zote hadi kuvuna, licha ya kuuza mbolea zetu tunatoa ushauri kumsaidia mkulima kufikia malengo yake ya kuvuna kwa tija, alifafanua Msuya.
Msuya ameongeza kuwa kwa kuona umuhimu wa kuelimisha na kutatua changamoto za wakulima shambani, wamesajili mbolea aina 11 ambapo aina 9 kati ya hizo zipo sokoni na zinafanya vizuri, zikizingatia mahitaji ya mkulima na zimegawanyika katika makundi manne muhimu.
No comments
Post a Comment