Zinazobamba

Veta Mtwara inavyotoa fursa ya kuchonga Vinyago kwa Vijana.


Na Mwandishi Wetu.

Chuo Cha Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) Mtwara kwa kushirikiana kituo cha Sanaa na Uchumi Afrika(ADEA)kimekua kikiwakusanya Vijana wenye umri wa miaka 9,10,11 hadi 12 na kuwapatia Mafunzo ya ujuzi wa kuchonga vinyago mbalimbali. 

Hayo yamebainishwa Julai 4,2025 Jijini Dar es salaam  na Msanii mahili kutoka Chuo hicho Saidi Chilumba wakati akizungumza na Waandishi wa Habari waliotembelea bandi la VETA  katika maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba  
"Wewe kama ni mtengenezaji wa kitanda chonga na kinyago,ukiwa unasubiri mteja wa kitanda sasa unao uwezo mwingine wa mimsubiri mteja wa kinyago."amesema Chilumba 

Nakuongeza kuwa" Lakini pia tumeongezea thamani kwenye vitu mbalimbali Kwa mfano tunatengeneza henga za nguo(Hooks) mafundi wa kuchomelea wanatupa baadi ya vipande vya  chuma  ambavyo wanaona wao  havina thamani, kwahiyo sisi tunavigeuze tunatengeza structure kama ya kipepeo kama unavyoona,tumechora tingatinga."
Anasema Kipande hiki ukienda kwa fundi chuma ambaye amekipoteza ambapo ukienda kuuza inawezekana ukapata mia tano(500),lakini sisi baada ya kukiboresha kukiongezea thamani hii sanaa saivi tunauza elfu 25.

Anasema fikiria kutoka shilingi 500 hadi elfu 25,tayari tumeshatengeneza fursa ya ajira kwa Vijana ambao walikua wanadhurula mitaani,wengine ambao hawajaenda VETA,tumewakusanya kwa ule ujuzi ambao tumeupata VETA tumekuaa tukiwapa Vijana hawa wajue zile bidhaa ambazo zilikua za kawaida sasa zimeanza kuwa ni thaman
"Kwa mfano hapa kuna kifuu cha nazi,ukipita mtaani wakina mama wanakuna nazi nakutupa vifuu vya nazi kila sehemu,sasa sisi tumegeuza fursa ya kifuu cha nazi sasa imekua bidhaa,nazi unaweza kuinunua shilingi 500 au 100,lakini sisi tulipotengeneza hii sanaa tumeipamba vizuri,tumeichora saivi hii hapa tunauza elfu 30.

Kwahiyo sisi kazi yetu nikuongezea thamani kwenye vitu ambavyo jamii inaona nivya kawaida,lakini pia tumegundua kwamba kuna haja ya kutengeneza vizibo vya chupa ya Wine,tumetengeneza kizibo ambacho ni standadi kwa kutumia mpingo na kifaa tumeweka chini kinaitwa koku,ukishaunganisha ukifunga tayari umepata kizibo cha chupa ya Wine.
Haya haya ni matumizi ya rasilimali ambazo Watanzania tunazo ambapo tunauwezo wa kutumia nakutoa ajira kwa Vijana,kupitia maonesho kama haya tunajitahidi kutoa Elimu kwa jamii kwamba VETA ni sehemu rafiki ya kuja kupata Mafunzo ndio maana kauli mbiu ya VETA inasema "VETA FURSA KAMA ZOTE"





No comments