TANESCO YATANGAZA KAMPENI KUHAMASISHA ULIPAJI WA MADENI KWA WATEJA WAKE.
Kaimu Mkurugenzi Mawasiliano na huduma kwa wateja Irene Gowelle.
Na Mussa Augustine.
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania(TANESCO) imetangaza kuanza kwa kampeni maalum nchini ya kuhamasisha ulipaji wa madeni kutoka kwa wateja wakubwa nawa kati wa malipo ya baada,pamoja na ukaguzu wa mita za LUKU kwa wateja wa malipo ya kabla.
Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 19,2025 Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na huduma kwa Wateja TANESCO ,Irene Gowelle wakati akizungumza na Waandishi wa habari nakubainisha kuwa kampeni hiyo imeanza rasmi leo Juni 19,2025 nakwamba kampeni hiyo itakua endelevu.
Aidha mesema kwamba malengo ya kampeni hiyo ni kuhamasisha wateja wa malipo ya baada kulipa madeni yao kwa hiyari kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa,pamoja kutoa motisha kwa ulipaji wa wakati ikiwemo msamaha wa riba kwa wateja watakaolipa madeni yao kikamilifu.
"Kampeni hiyo imepewa jina la "Lipa deni,Linda Miundombinu,Tukuhudumie",ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha ulinzi wa miundombinu ya umeme pamoja na juhudi za kuboresha na kuimarisha uendelevu wa upatikanaji huduma bora ya umeme kwa wananchi."amesema Gowelle
Nakuongeza kuwa" Zoezi hili pia litahusisha ukaguzi wa mita za LUKU kwa lengo la kuhakikisha zinafanya kazi vizuri na hazijachezewa na wateja wasio waaminifu,na kauli mbiu yake ni" Huduma endelevu huanza na wewe.'
Aidha,Gowelle amesema kuwa TANESCO inawahamasisha wateja na Wananchi kwa ujumla kutambua umuhimu wa ulinzi shirikishi wa miundombinu ya umeme kwa kuwajumuisha wananchi na kuwapa elimu ya kulinda miundombinu ya Shirika.
"Miundombinu hii ndio inayowezesha upatikanaji endelevu wa huduma ya umeme kwa ufanisi hasa kwa kuzingatia kuwa ulinzi wa Miundombinu ya umma ni wajibu kila mwananchi"amesisitiza Gowelle
Hata hivyo Shirika hilo la Ugavi wa Umeme kupitia Kamu Mkurugenzi wa Mawasiliano na huduma kwa Wateja Irine Gowelle limetoa rai kwa wateja wake wote nchini ambao wanadaiwa kutoa ushirikiano kwa kulipa madeni yao kwa wakati ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza pindi itakapotokea ukosefu wa upatikanaji wa huduma ya umeme kwenye shughulu zao.
Halikadhalika Shirika hilo limewaomba Wananchi kutoa taarifa kuhusu vitendo vya wizi wa umeme au uharibifu na wizi wa miundombinu ya umeme kwa kushirikiana na Vyombo Vya dola ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kwa ukosefu wa huduma ya umeme pamoja na kuzuia hasara kwa Shirika.
Post Comment
No comments
Post a Comment