ISMAIL SALUM ATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.
Na Mussa Augustine.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema leo Juni 18,2025 Jijini Dar es salaam Salum amesema kwamba ameamua kugombea nafasi hiyo ili kuhakikisha anawaletea maendeleo wananchi wa Jimbo la Kahama mjini.
"Uchaguzi wa Mwaka huu ndani ya CCM umekua umeboreshwa ambapo kura zinapigwa kumpitisha Mgombea kuanzia kuanzia ngazi ya Shina,tofauti na hapo awali ambapo walikua wanategemewa wajumbe pekee kutoa maamuzi kwenye vikao"
Katika hatua nyingine Mgombea huyo wa Ubunge kupitia CCM katika Jimbo la Kahama Mjini amekemea vitendo vya uvunjifu wa amani ambavyo vinafanywa na viongozi wa Chama Cha demokrasia na Maendeleo( CHADEMA )kupitia kauli mbiu ya "Hakuna mabadiliko,hakuna Uchaguzi" (No Reforms no Election)
"Nimekua nawashangaa wana Chadema ambao wanasema eti bila mabadiliko hakuna uchaguzi, hizi ni kauli za uchochezi ambazo zinatafsirika kwamba wanataka kuwepo wa uvunjifu wa amani, hivyo hatuwezi kukubaliana na hilo" amesema Salum
Nakuongeza kwamba"Nawaomba Watanzania wajitokeze kwenye kushiriki uchaguzi Mkuu,waachane na hizo propaganda zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii ambazo zinasababisha taharuki kwenye Taifa letu" amesema.
No comments
Post a Comment