WILSON ELIAS ACHUKUA FOMU KUGOMBEA NAFASI YA URAIS KUPITIA TLP.
Mgombea Urais kupitia chama cha TLP Wilson Elias akionesha begi lenye fomu ya kugombea nafasi ya Urais
Na Mwandishi Wetu.
Mfanyabiashara Wilson Elias amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Tanzania Labor Party ( TLP) huku akijinasibu kuinua uchumi wa Watanzania endapo atashinda nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Akizungumza leo Mei 8,2025 mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu Mkuu TLP Yustus Rwamugira Jijini Dar es salaam,Mtia nia huyo amesema kwamba ameamua kugombea nafasi hiyo kutokana nakwamba anauwezo mkubwa wa kusimamia rasilimali za nchi ili ziwanufaishe Watanzania wote.
Mgombea Urais kupitia TLP(mwenye koti la rangi nyeusi) Wilson Elias akionesha fomu ya kuongombea nafasi hiyo,kushoto kwake ni katibu Mkuu wa TLP Yustus Rwamugira."Mimi(Wilson Elias)ni mtia nia wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika chama Cha TLP, sababu za kugombea ninazo,nia ya kugombea ninayo,na uwezo ninao."amesema Elisha
Nakuongeza kuwa"Vpaumbele vyangu vya kwanza ni kwenye uchumi,mimi ni mtu ambaye nina uzoefu kwenye uchumi,nimezunguka na kufanya utafiti katika nchi mbalimbali duniani."
Amesema kuwa anauzoefu katika nyanja zote hasa kuinua Maisha ya Mtanzania, kuinua sekta za Elimu,Afya,Miundombinu ya Barabara,pamoja na nyanja zote ambazo zitamrahisishia mwananchi kumuondoa katika hali ya umaskini ambayo ni janga kubwa katika Taifa.
Mgombea Urais kupitia TLP Wilsoni Elias (mwenye mkoti wa rangi nyeusi) akiwa na Katibu Mkuu TLP Yustus Rwamugira wakati wa makabidhiano ya fomu ya kugombea nafasi hiyo.Mtia nia huyo wa nafasi ya urais TLP amekiri kuwa Serikali iliyopo madarakani inaongoza vizuri,nakudai kuwa yeye ataifikisha Tanzania katika viwango ambavyo ni tofauti na hali ilivyo kwa sasa,.
"Ukifuatilia nchi yetu imebarikiwa rasilimali nyingi ikiwemo Madini,sasahivi Mkoani Mbeya kuna Madini ya kimiminika yanayojulikana kama Madini ya Helium,ambayo ni muhimu zaidi,dunia saivi ina mapungufu ya Madini ya Helium lakini yanapatikana kwetu Tanzania,hivyo hizi rasilimali lazima niweze kuzisimamia ziweze kumnufaisha Mtanzania mmoja mmoja."amesema
Amesema kuwa ana uwezo wa kufanya kampeni kwa maana ya kushindana na vyama vingine,kutangaza sera za TLP nchi nzima pia amefanya tafiti mbalimbali akitolea mfano kwenye sekta ya Nishati,akidai kuwa nchi nyingi kwa sasa zinatumia Nishati ya jua,hivyo Tanzania ina Mikoa ya kanda ya kati ambayo inazalisha umeme wa jua na hatimaye kupunguza bei ya Nishati ya umeme ili Watanzania wa kawaida waweze kunufaika.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wilson Elias akizungumza na Waandishi wa habari(hawapo pichani) mara baada ya kuchukua fomu.Elias ambaye ni mzaliwa wa Mkoani Tanga pia amezungumzia sekta ya Maji nakudai kuwa bado kuna tatizo la Maji nchini humo,nakufafanua kuwa dunia imetoka katika uchimbaji wa mabwawa au kutegemea mito,kwa nchi zote zenye bahari kwa mfano nchini Misri na nchi za falme za kiarabu zina tumia njia ya kuvuna Maji ya bahari kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya nyumbani.
"Kwahiyo tunaweza kuvuna Maji kwa maeneo yote ya Dar es salaam mfano Kigamboni na maeneo yote bahari inapozunguka,tunapaswa kuondokana na vyanzo vilivyopitwa na wakati kwa kutegemea mito ambayo kutokana na mabadiliko ya Tabianchi tumeona matatizo ya upatikanaji wa Maji hasa kwenye Jiji letu la Dar es salaam."amesema
Awali Katibu Mkuu wa TLP, Yustus Rwamugira, amesema mchakato wa kuchukua fomu za urais ndani ya chama hicho utaendelea hadi mwishoni mwa mwezi huu na mchujo wa kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho utafanyika baada ya Bunge kuvunjwa.
WILSON ELIAS ACHUKUA FOMU KUGOMBEA NAFASI YA URAIS KUPITIA TLP.
Reviewed by mashala
on
15:25:00
Rating: 5
Reviewed by mashala
on
15:25:00
Rating: 5



No comments
Post a Comment