Zinazobamba

NLD YASIKITISHWA NA IDADI NDOGO YA WANANCHI KUJIANDIKISHA KUPIGA KURA SERIKALI ZA MITAA

Leo, Oktoba 17, 2024, Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe Doyo Hassan Doyo, alihudhuria katika zoezi la kujiandikisha katika daftari mpiga kura mkazi katika kata ya Mabada, mtaa wa Kwedigongo, Handeni Tanga, katika shule ya msingi Kwediziwa.

Aidha, Mhe. Doyo alionyesha kusikitishwa na idadi ndogo ya wananchi wanaojitokeza kujiandikisha katika daftari mkazi, huku alitoa wito kwa TAMISEMI kuongeza juhudi za uhamasishaji ili wananchi wengi waweze kujitokeza na kupata nafasi ya kujiandikisha katika daftari hilo, na hatimaye kupata fursa ya kupiga kura katika  uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji.

Pia Mhe. Doyo alizungumzia umbali wa vituo vya kujiandikisha, akihimiza TAMISEMI kuongeza vituo ili kupunguza umbali wa kwenda kujiandikisha. katika na kituo na kituo, inachukua kilomita 1, kuna haja ya TAMISEMI kuweka vituo karibu zaidi ili kuondoa vikwazo vinavyoweza kumpa mtu sababu ya kutokwenda kujiandikisha" alisisitiza Mhe. Doyo. "Hii inaweza kuwa sababu moja wapo ya watu kushindwa kujiandikisha.

Hakuna maoni