Zinazobamba

WAKULIMA MKOANI MANYARA WAVUTIWA NA MBOLEA ZA AGRAMI AFRIKA.



Na Mwandishi Wetu.

Baadhi ya wakulima waliotembelea maonesho ya mbolea mjini Babati mkoani Manyara wamesema kati ya vitu vilivyowavutia ni mbolea za aGrami zenye sifa tofauti ikiwemo kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Wakizungumza wakati wa maonesho ya mbolea yalimalizika mjini Babati wakulima hao wamesema wamepata elimu ya kutosha kuhusu kurekebisha nyongo kwenye maji kabla ya kutumia mbolea za kimiminika au viuatilifu, walipotembelea aGrami Afrika kwenye maonesho hayo katika banda la kampuni ya Bens.

Akifundisha wakulima waliotembelea banda hilo afisa kilimo wa kampuni ya aGrami Afrika Salim Msuya amesema wakulima wanapaswa kutambua kiasi cha tindikali au nyongo kwenye maji wanayotumia kumwagilia au kuchanganya viuatilifu au mbolea za maji, kwa kutumia mbolea aina ya MI6.1 inayopatikana aGrami.

Msuya amesema kwa kutumia mbolea aina ya MI6.1 kutoka aGrami Afrika mkulima atapata faida zaidi ya moja ikiwemo kurekebisha tindikali ya maji anayotumia wakati husika na kupata virutubisho vya nyongeza vinavyosaidia kuchochea ukuaji wa mmea, kuchochea ufyonzaji wa madini yaliyopo ardhini na kusaidia kupunguza msongo wa mmea.

Msuya amezitaja baadhi ya mbolea kutoka kampuni ya aGrami zilizopo sokoni na zilizosajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuwa ni energy Mix ambayo ni mbolea mama yenye virutubisho muhimu Nitrojeni, Phosphorus na Potasiamu (NPK)

MI6.1, BorMI, MIzboze, Cynk(zinc) Wapn yenye wingi wa calcium nanoMI Silver, nanoMI Copper n.kamewata


ka wakulima kuzingatia kanuni bora za kilimo, uchaguzi sahihi wa mbolea ikiwemo kutumia mbolea za kupandia na kukuzia mbolea za aGrami ili kupata matokeo mazuri ya mavuno.

Msuya ameeleza upatikanaji wa mbolea hizo na matumizi yake kuwa ni rahisi kupatikana na rafiki wa mazingira na mtumiaji pia,  kuwapa mwito wakulima kujenga tabia ya kujifunza teknolojia mpya za kilimo ili kupata tija.

Kampuni za aGrami Afrika na Mzuri Afrika zinawafikia wakulima na kuwapa elimu kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo maonesho ya wakulima sabasaba, nanenane, maonesho ya siku ya mbolea duniani, kupitia mashamba darasa na vyombo vya habari, wakiongozwa na kauli mbiu yao Sayansi haiongopi tukutane shambani na Ufanisi kupitia maarifa

Kampuni ya mbolea ya aGrami Afrika inaingiza mbolea zake kutoka nchini Poland zikitajwa kuleta matokeo chanya kutokana na teknolojia iliyotumika kutengeneza mbolea, sambamba na kampuni tanzu ya Mzuri Afrika inayojihusisha na uingizaji wa mashine inayorahisisha utendaji kazi wa mkulima ikiwa na uwezo wa kulima, kulegeza udongo, kupanda na kuweka mbolea kwa wakati mmoja.

Hakuna maoni