Zinazobamba

RAIS DTK.SAMIA MGENI RASMI JUBILEE YA MIAKA 50 YA AICT MAGOMENI.

Na Mussa Augustine

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi Jubilee ya Miaka 50 ( Golden Jubilee) ya kanisa la AICT - Postoret ya Magomeni itakayofanyika Oktoba 27 ,2024.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Askofu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Pwani ,Askofu Philipo Magwano Mafuja wakati azikungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam.

Aidha Askofu Mafuja amesema kuwa siku ya maadhimisho hayo itafanyika ibada ya misa maalumu ya kumtukuza, kumsifu,kuabudu na kumuomba Mungu.

"Tunayo furaha kubwa kuwataarifu waumini wote wa ACIT na Watanzania kwa ujumla kuwa Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekubali kujumuika nasi kwenye misa hiyo,itakayoenda sambamba na harambee ya kukamilisha ujenzi wa kanisa unaoendelea kanisani hapa ambayo yeye ndiye mgeni rasmi" amesema

Nakuongeza kuwa,"tunayo furaha kuwataarifu mamilioni ya waumini wa kanisa la AICT kila mahali nchini,lakini pia kanisa la AIC katika nchi kukualika ujumuike nasi katika ibada ya Misa maalumu ya kusherehekea jubilee ya Miaka 50 ya kanisa letu pendwa tangu lilipoanzishwa na kuanza kutoa huduma.

Aidha ameendelea kusisitiza kuwa shughuli hiyo ni tukio la furaha kuadhimisha miaka 50 ya uaminifu wa Mungu kwa kusanyiko la kanisa la AICT Magomeni ambalo ni sehemu ya kusanyiko kubwa la waamini wa kanisa la Africa Inland Church -Tanzania (AICT).

"Tutajiskia Faraja kubwa Watanzania wenzetu wa madhehebu mbalimbali wakija kujumuika nasi kwenye ibada ya Misa maalumu,tunapoadhimisha wakati huu muhimu katika historia ya kanisa letu,itakua ni fursa adhimu na adimu ya kuungana na marafiki wa zamani,kufurahia katika imani yetu ya pamoja na kufikiria mustakabali wa kanisa letu" amesema Askofu huyo.
Aidha amebainisha kuwa kuelekea siku hiyo ya tarehe 27 Oktoba 2024 kutakuwa na shughuli zingine mbalimbali ikiwemo Tamasha la uimbaji,Maombi,na shughuli za kijamii namatendo ya huruma na upendo kwa jamii ya Watanzania akitolea mfano ugawaji wa mitungi ya gesi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia katika agenda ya nishati safi na kutembelea  Vituo vya watoto yatima kuwajulia hali na kushirikiana.




Hakuna maoni