Zinazobamba

MBWAMA AHIMIZA WAFANYABIASHARA SOKO LA MABIBO KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA KUPIGA KURA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Na Mussa Augustine.

Meneja wa Soko la Ndizi lililopo kata ya Mabibo Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam, Bw.Geoffrey Mbwama amewaomba wafanyabiashara wa soko hilo pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura la serikali za Mitaa.

Ametoa wito huo leo Oktoba 11, 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake sokoni hapo,nakusema kuwa tayari Maafisa waandikishaji wamefika sokoni hapo na kutoa Elimu kuhusu zoezi la kujiandikisha katika daftari la wapiga kura la Serikali za Mitaa.

"Tunaendelea kutoa matangazo kwa wafanyaibaishara washiriki kujiandikisha ili wapate haki zao za msingi za kupiga kura na kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa ambao ndio msingi wa Maendeleo katika maeneo yao" amesema Meneja Mbwama

Akizungumzia kuhusu uboreshaji wa miundombinu ya soko Mbwama amesema kuwa kwa sasa ujenzi wa barabara ya Ndizi Mbeya yenye urefu wa Mita 150 ,upo katika mchakato wa kufanya tathmini na mahesabu nakwamba fedha tayari zimeshatengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo.

"Barabara hii inasababisha tope,Sasa tupo kwenye hatua ya kufanya tathmini ili ujenzi uanze mara moja,ujenzi utakua wa kiwango cha zege na tunategemea kuanza mwezi huu wa kumi,na endapo tutakamilisha basi tutakua tumeondoa adha kubwa ilivyokua ikiwakumba Wafanyabiashara.
Kuhusu matumizi ya Nishati Safi sokoni hapo,meneja huyo amesema mamalishe na babalishe wapatao 80 kati ya 105 wamepatiwa mitungi ya gesi yenye kilo 15 ili kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutaka Nishati safi itumike kwenye masoko yote Nchini ili kuepusha athari za kiafya na kimazingira.








Hakuna maoni