Zinazobamba

BALOZI DKT.CHANA AWAHIMIZA WATANZANIA KUHIFADHI RASILIMALI ZA NCHI.

                    Balozi Dkt.Pindi Chana

Na Mussa Augustine.

Waziri wa Maliasiri na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chama amewahimiza Watanzania  kuzitunza na kuhifadhi rasilimali zilizopo Nchini ili kuendelea kukuza sekta ya Utalii.

Balozi Dkt Chana ametoa rai hiyo leo Oktoba 13,2024 Jijini Dar es salaam wakati akifunga onesho la nane la Utalii la Kimataifa la Swahili ( S!TE) ambalo limefanyika kuanzia Oktoba 11 ,2024 katika ukumbi wa Mlimani City 

Amesema kuwa kuwa utalii na ulinzi wa rasilimali za Nchi yetu ni kipaumbele Cha Kila mtanzania,hivyo hakuna budi kuhakikisha kila mtanzania anafanya hivyo ili kukuza eekta ya utalii Nchini.

Aidha amesema kuwa sekta ya Utalii inachangia asilimia 17 za pato la Taifa(DGP),huku ikingiza fedha za kigeni ni asilimia isiyopungua 25,ambazo ni zaidi ya Dola bilion 3.

"Tukizungumzia suala la utalii kila mtu ananufaika,kwanza shirika la ndege ATCL linapata abiria wengi wanaokuja kutalii nchini hapa,,pia mtalii anaposhuka anatumia usafiri wa ndani ambapo madereva wananufaika,hivyo hivyo ananunua bidhaa mbalimbali,hata mkulima mdogomdogo huko kijijini ananufaika kwa uuza mazao yake,huu ni  mnyororo mkubwa wa thamani katika sekta ya Utalii." Amesema 

Nakuongeza kuwa Tanzania tuna vivutio vingi ,kuna Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote Afrika Mashariki, tuna Utalii wa fukwe,mali kale, pia tuna hifadhi za National Parks zisizopungua 21, makumbusho za Taifa  zisizopungua saba.

Balozi Dkt Chana amesema kuwa kadri siku zinavyokwenda watalii wanazidi kuongezeka ambapo kauli mbiu ya onesho la S!TE  mwaka huu " Utalii na Amani" ambapo Tanzania ni kisiwa Cha amani na imekua mfano katika nchi za Afrika Mashariki na  SDAC.

Hata hivyo Balozi Dkt. Chana ametumia fursa hiyo kuwashukuru Watanzania kwa kuendelea kudumisha amani na utilivu pamoja  na kuendeleza kudumisha mila na desturi za kitanzania  kwani imekua chachu kubwa ya kuvutia watalii.
               Balozi Dr. Ramadhan Dau
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanazia (TTB) Balozi Dr. Ramadhan Dau amesema kuwa onesho la mwaka huu limepata mafanikio makubwa ukilinganisha nala Mwaka Jana kutokana na wanunuzi wa vifaa vya Utalii kuongezeka,makampuni ya kufanya maonesho,

"Kama alivyosema waziri,kwenye utalii kuna mambo mawili ,kwanza kuhifadhi,pili kutangaza utalii,na sisi TTB kazi yetu kubwa ni kutangaza utalii nje ya nchi na hata kwa watanzania wenyewe,lakini pamoja na hili la uhifadhi kua  lipo kwenye Wizara yetu lakini ni jukumu la kila mtanzania kuhifadhi rasilimali" amesema Balozi Dr.Dau



Hakuna maoni