Zinazobamba

WATAALAMU WA UMEME UKANDA WA SADAC WAKUTANA KUJADILI MIKAKATI YA KUSAFIRISHA NISHATI HIYO.

Na Mwandishi wetu

Wanachama  wa Jumuiya za Nchi za kusini mwa Afrika (SADC), katika nyanja ya umeme wamekutana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati endelevu ili kufufua vyanzo vya nishati hiyo kwa lengo la kufanikisha kusafirisha na kusambaza kwa wateja wa ukanda huo.


Akizungumza katika mkutano huo, leo Oktoba 15 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Dkt Khatibu  Kazungu , amesema wataalamu wa umeme kutoka Jumuia hiyo wamekutana kwa lengo la kujadili na kutatua changamoto wanazokutananazo ili wafikie malengo mahususi.


“Lengo la mkutano huu wa wataalamu wa umeme wa Jumuia ya SADC ni kuweka mikakati madhubuti ya kutumia vyanzo vilivyopo ili kushirikiana kwa pamoja katika kufufua umeme, kusafirisha na kusambaza kwa wateja.


“Sisi kama Serikali tuna mradi unaoitwa TAZA, wenye lengo la kuunganisha miundombinu ya umeme hapa Tanzania na Zambia na tunapokutana katika vikao kama hivi tunapitia mikakati hiyo na hatua ambayo tumefikia na kutua changamoto zinazotukwamisha kufikia malengo hayo, ” amesema.


Pia ameongeza kuwa, mahitaji ya umeme wa ndani huko vizuri kutokana na kuwepo kwa mradi wa Bwawa la Nyerere ambalo kwa sasa linauwezo wa kuzalisha megawati 700 na siku chache zijazo litazalisha megawati 900.


Amebainisha kwamba tofauti na Bwawa la Nyerere pia kuna vyanzo vingine kikiwemo cha mradi wa Umeme wa Jua, ambao kwa sasa una uwezo wa kuzalisha megawati 600 na kupitia Joto Ardhi nako kunazalishwa umeme megawati 5000 na kufanya Tanzania isiwe na tatizo la uzalishaji wa umeme na kinachotakiwa ni kujipanga vizuri kama Serikali kuongeza vyanzo vingine.


“Serikali pia ina mradi mwingine wa umeme unaoitwa Green Imara ambao ni mahususi katika kuboresha miundombinu ya umeme na kuingeza vyanzo vingine na kuunganisha nishati hiyo katika mikoa ya pembezo mwa nchi ambayo Katavi, Kigoma, Lindi na Mtwara hadi mwisho wa mwaka huu itakuwa imeeinguzwa katika gridi ya Taifa,” amesema.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji uzalisahi umeme TANESCO,  Mhandisi Costa Rubagumya, amesema Tanzania iko katikati ya ‘East Africa Powe Pool’ ambako inapatikana Kenya na kwa upande wa ‘Southern African Power Pool’ inapatikana Zambia.

“Katika maeneo hayo mawili inatupa uwezekano wa kusaidiana katika nyanja ya umeme ikiwa nchi mojawapo inapokuwa na shida ya nishati hiyo, mfano eneo la Kariba kwa sasa lina ukame na kusababisha Zimbabwe na Zambia kupitia katika kipindi kigumu na kutokana na kuwepo kwa ushirikiano huu unatoa fursa ya kusaidiana na kutuweka salama katika nyanja ya umeme,” amesema.

Hakuna maoni