DOYO HASSANI DOYO APINGA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU,ADAI MATOKEO HAYO NI BATILI,AKATA RUFAA.
Doyo Hassan Doyo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)
Shaaban Itutu ,ambaye Mwenyekiti Mpya aliyeshinda kwenye uchaguzi
Na Mwandishi Wetu.
Doyo Hassan Doyo ametoa matamshi hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,nakusisitiza kuwa hatambui uchaguzi huo uliofanyika June 29 mwaka huu Jijini Dar Es Salaam,huku akimtupia lawama aliyekuwa mwenyekiti wa Chama hicho Hamad Rashid kwamba amevunja kanuni za uchaguzi wa chama hicho za mwaka 2019..
Doyo amesema yeye pomoja na wanachama wengine zaidi ya 70 tayari wameshakata rufaa ya kupinga matokeo hayo kwenye kamati ya rufaa ya ADC ili kupata haki ambayo hawakuipata katika Uchaguzi huo ambao amedai uligubikwa na sintofahamu kubwa ikiwemo vitendo vya rushwa.
"Jana saa 10 kasoro tulipeleka notisi kwa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi na dakika chache baadaye tukawasilisha rufaa ya kupinga matokeo Kwa mujibu wa kanuni za chama chetu kwani aliyekuwa Mwenyekiti Wetu Hamad Rashid alivunja kanuni za uchaguzi na anataka kukigeuza chama kuwa kikundi Cha familia yake"amesema Doyo.
Akizungumza kuhusu sababu kuu zilizomfanya kuyakataa matokeo ya uchaguzi huo na Kukata rufaa amesema kuwa ni pamoja na kitendo Cha Hamad Rashid kungoza kikao kama Mwenyekiti wa muda na kusimamia tangu mwanzo Hadi mwisho wa zoezi la uchaguzi bila hata kumtangaza mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Jambo ambalo limekwenda kinyume na katiba ya Chama hicho ya mwaka 2019.
"Haiwezekani Msimamizi wa muda wa uchaguzi amekaa pale ukumbini mpaka saa 3 usiku na haya ninayoyaongea,bahati nzuri Naibu msajili wa vyama vya Siasa aliyashuhudia maana alikuwepo pale,Hamad Rashid ndiye aliyeongoza mkutano mkuu,Kwa hiyo Kwa Habari ya kuvunjwa kwa katiba ameshuhudia Naibu msajili kuwa aliyesimamia Mkutano hakuwa anatakiwa kusimamia "amesema Doyo.
"Mimi Nina Kadi namba 2 ya chama yaani ni miongoni Mwa waaasisi wake Sasa Leo mtu asije akataka kukigeuza chama kama genge la familia yake,chama hichi na Cha wote na sijakata rufaa Kwa kuwa eti nimeshindwa uchaguzi Bali ni Kwa sababu Katiba ya Chama ilivunjwa katika zoezi Zima la uchaguzi"amesema.
Kwa upande wake aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Makamo mwenyekiti wa ADC, Zanzibar Bi Shara Amrani Hamis amemshushia lawama aliyekuwa mwenyekiti wa Chama hicho Hamad Rashid Kwa kutowapa Wapiga kura faragha na badala yake baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi walikuwa wakiwafuata Wapiga kura wakati zoezi la upigaji kura likiendelea wakiwaambia wamchague Fulani katika uchaguzi huo.
Bi Shara ameongeza kuwa Hamad Rashid alimpigia simu kutaka asigombee nafasi hiyo ili nafasi hiyo agombee mtoto wake Jambo ambalo ni kinyume Cha taratibu,kanuni na katiba ya chama ambayo inampa mwanachama yoyote fursa ya kugombea.
Halikadhalika Mwenyekiti wa Vijana wa Chama hicho amesema kuwa wamekata rufaa ya kukukataa uchaguzi huo kwani ulitawaliwa na nguvu za Mwenyekiti aliyemaliza muda wake huku baadhi ya watu akiwemo yeye kuahidiwa kupewa vyeo ili kuzibwa midomo Jambo ambalo wamelikataa kwa kudai kuwa hawana uchu wa madaraka na wanataka haki itendeke.
Amesema wanaamini kuwa kamati ya uchaguzi itatenda haki kwani ushahidi wote wa jinsi kanuni za Uchaguzi huo ulivyokiukwa unaonekana dhahiri.
No comments
Post a Comment