RAIS NYUSI WA MSUMBIJI KUFANYA ZIARA YA SIKU NNE TANZANIA
Na Mussa Augustine.
Rais wa Msumbiji Philip
Jacinto Nyusi anatarfajwa kuwasili Nchini Tanzania kwa ziara yake ya kikazi ya siku nne kuanzia
Julai 1 hadi 4 ,2024 ikiwa ni muendelezo wa
mahusiano ya nchi hizo mbili yaliyodumu kwa muda mrefu.
Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 30,2024, jijini Dar es Salaam na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh.Januari Makamba wakati
akizungumza na waandishi wa habari nakubainisha kuwa Rais Nyusi anatarajiwa kuwasili
nchini Tanzania kufuatia mwaliko maalumu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
Samia Suluhu Hassan.
Waziri Makamba amesema
kuwa Rais Nyusi ndie anaetarajiwa kuwa mgeni rasmi atakayefungua maonyesho ya
48 ya biashara ya kimataifa (Saba saba) Julai 3, 2024 baada ya hapo ataelekea
Zanzibari.
“Ukiangalia kuna raia wa Msumbiji wapo Tanzania wakifanya shughuli zao za kiuchumi ,na sisi Watanzania wapo Msumbiji wakifanya shughuli za kiuchumi hivyo siyo jambo la kushangaza kuendelea kudmisha ushirikiano na uhusiano wetu ambao umekuwa wa muda mrefu sasa”amesema Waziri Makamba.
Nakuongeza kuwa “Ziara
hiyo itaanzia pale Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Julai 1 ,atapokelewa na
Viongozi wa mbalimbali na tarehe 2 atakutana na Rais Samia Suluhu Hassan ikulu,
ambapo watafanya mazungumzo ya faragha watajadili mambo mengi ikiwemo ushirikiano
wa kibiashara kati ya nchi hizi mbili ili kuimarisha mahusiano yetu.
Aidha Waziri Makamba pia amesema katika ziara hiyo mikataba kadhaa itasainiwa ambapo itahusu ushirikiano katika Sekta Mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya, Elimu , Madini pamoja na Habari lengo ni kuongeza mahusiano mazuri hususani katika kuimarisha ulinzi na usalama baina ya nchi hizo mbili hususani maeneo ya mpakani
No comments
Post a Comment