Kiwanda cha Kibaiolojia kinachomilikiwa na serikali cha Tanzania Biotech Product limited (TBPL) kilichoko Kibaha mkoani Pwani
Na Mwandishi Wetu
Kiwanda cha
Kibaiolojia kinachomilikiwa na serikali cha Tanzania Biotech Product limited
(TBPL) kilichoko Kibaha mkoani Pwani kimeingia rasmi mkataba wa miaka mitatu na
kampuni ya JJ Agricultural Ltd ya kusambaza ,
dawa mpya za viuatilifu hai ambavyo
vitatumika katika kupambana na wadudu dhurifu wa mazao mbalimbali ya kilimo
ikiwemo mazao ya pamba, Mahindi, matunda pamoja na mbogamboga hali
itakayosaidia kupatikana kwa dawa hizo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kwa Mujibu wa Taarifa
iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Masoko,Shirika la Taifa la Maendelo
(NDC),Mkataba huo umesainiwa Machi
19,2024 kiwandani hapo Kibaha mkoani Pwani ambapo kwa upande wa kampuni ya TBPL
imewakilishwa na Meneja Mkuu wa kiwanda hicho Rafael Rodriquez wakati kwa
upande wa JJ Agricultural Ltd imewakilishwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo
Mhandisi, James Kilaba.
Akizungumza mara baada
ya kukamilika kwa zoezi la kutiliana saini mkataba huo Meneja Mkuu wa kiwanda
hicho, Bw. Rafael Rodriquez ameonyeshwa kufurahishwa na makubaliano waliyofikia
na kampuni ya JJ Agricultural Limited ambapo amebainisha kuwa hatua hiyo ni
mafanikio makubwa katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata fursa ya kufikiwa
na bidhaa hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.
“Tunatambua changamoto
inayowakabili wakulima ya uwepo wa wadudu dhurifu katika mazao yao makabaliano
haya yanakwenda kuwasaidia wakulima katika kupatikana kwa dawa hii hali
itakayowafanya wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika mazao yao”
amebainisha Bw. Rodriquez
Bw. Rodriquez pia
ametumia fursa hiyo kubainisha sifa za kipekee za dawa hizo za viuatilifu kuwa
ni tofauti na dawa zingine zinazopatikana sokoni kwa kuwa zenyewe
zimetengenezwa kwa namna ya viuatilifu hai ikilinganishwa na dawa zingine
zisizo za kibaolojia kwa kuwa zinapelekea madhara watumiaji kama vile magonjwa
ya kansa pamoja na kuharibu mazingira huku akiwataka mawakala zaidi kuendelea
kujitokeza kwa wingi.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa kampuni ya JJ Agricultural Ltd, Mhandisi James Kilaba ameishukuru
TBPL kwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba huo huku akiomba kupewa
ushirikiano katika kipindi chote cha utekelezaji wake ambapo miongoni mwa kazi
zitakazofanywa na kampuni hiyo ni pamoja na kuhakikisha wanaandaa mashamba
darasa katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambayo yatatumika katika kutoa
elimu kwa wakulima juu ya namna bora ya kutumia dawa hizo katika kupambana na
wadudu dhurifu katika mazao yao.
Mkataba huu utakuwa ni
wa miaka mitatu ambapo kwa kuanzia dawa hizo zinatarajia kupatikana katika
mikoa ya Dar es salaam Pwani, Morogoro, Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga,
Iringa, Dodoma Singida, Katavi pamoja na Tanga na utahusisha pia utoaji wa
mafunzo ya namna bora ya kutumia dawa hizi ambao utakuwa unafanywa na wataalam
kutoka katika kiwanda cha TBPL.
Kiwanda cha Kibaolojia
cha TBPL ni kiwanda pekee kilichopo nchini na barani Afrika ambacho
kinamilikiwa na serikali na kinazalisha dawa za kibaolojia hapa nchini ambapo
kinazalisha dawa za Viuadudu vya kupambana na Maleria (biolarvicides) ambapo
kwa sasa mara baada ya kubaini uwepo wa changamoto za wadudu dhurifu katika
kilimo imeanza rasmi uzalishaji wa dawa za viuatilifu hai vya kilimo
(biopesticides) ambavyo ni bora na rafiki wa mazingira.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni