Taasisi Ya Hakielimu Yaipongeza Serikali Kufuta Ada kidato Cha Tano na Sita
Na Mussa Augustine.
Taasisi ya Hakielimu imeunga mkono Mapendekezo ya Bajeti kuu ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali ya mwaka 2022-2023 kwa kutoa elimu bila malipo kidato cha tano na sita katika shule za Serikali,nakusema kwamba hatua hiyo itasaidia Vijana wengi wa kitanzania kupata elimu.
| Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hakielimu Dkt .John Kalage akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es salaam. |
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Dkt .John Kalage amesema hatua ya serikali kutoa elimu bure kwa kidato cha tano na sita itasaidia watoto zaidi ya laki Moja wa kidato cha tano na sita kunufaika na Elimu hiyo huku ikizingatiwa kuwa watoto wengi wanatoka katika familia zenye hali duni yakiuchumi.
Dkt.Kalage ameipongeza wizara ya fedha inayosimamiwa na Waziri Dkt.Mwigulu Nchemba kwa kupendekeza Bajeti hiyo katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuongeza fedha kwa Wizara ya elimu kutoka shilingi trilioni 5.3 mwaka 2021-22 hadi shilingi trilioni 5.64 kwa mwaka wa Fedha 2022-2023 na kusema ongezeko hilo litasaidia kukuza sekta ya elimu nchini.
Hata hivyo Dkt .Kalage ameishauri serikali kuongeza kiwango cha ruzuku kwa kila mwanafunzi shule za msingi kwa mwaka toka elfu 10000 hadi 25000,na kutoka elfu 25000 kwa wanafunzi wa sekondari kwa mwaka hadi elfu 55000 kwa mwaka kutokana na kupanda kwa gharaza za kimaisha.
Amendelea kufafanua kuwa Serikali imeonesha nia ya kutoa mikopo ya Elimu kwa wanafunzi walio katika vyuo vya Kati na ufundi ambapo kabla ya uamuzi huo Serikali ilikua inatumia zaidi ya shilingi Bilioni 500 kila mwaka kugharamia mikopo ya wanafunzi was Elimu ya juu ngazi ya vyuo vikuu.
" Uamuzi wa kuoanua wigo wa mikopo kwa vyuo vya Kati na ufundi tunauunga mkono kwani hii itatoa fursa kwa wanafunzi takribani 385,115 wanaomaliza kidato Cha nne na ambao wanashindwa kujiunga na kidato Cha tano kutokana na kuwa na ufaulu wa chini ,pia wastani wa wanafunzi 11551 wanaohitimu kidato Cha sita nakushindwa kujiunga na vyuo vikuu kwasababu ya kupata alama za chini katika mitihani yao" amesisitiza.
Kuhusu Matumizi ya Lugha ya Kiswahili Dkt Kalage amesema kwamba Lugha ya kingereza iendelee kufundishwa vizuri Kama lugha ya kigeni na biashara huku lugha ya Kiswahili ikitumika rasmi Kama lugha ya kujifunzia na kufundishia katika ngazi zote za Elimu kama Serikali ilivyopendekeza.
"Hakielimu tupo kwenye kampeni ya kuchagiza Matumizi ya Lugha Kiswahili katika kufundishia ili kuwawezesha wanafunzi kujifunzia kwa kina na kukuza umahiri unaokusudiwa Kama vile fikra tunduizi na ubunifu,lugha ya Kiswahili ikitumika Vijana wa kitanzania watakua na umahiri wakutosha kwenye maudhui kwasababu ndio lugha inayotumika kila saiku kwenye maisha yao" amesema Dkt Kalage.
No comments
Post a Comment