Ufahamu Ugonjwa Mokeypox
Ofisa wa shirika la afya
ulimwenguni WHO na mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza David Heymann amesema
kuwa ugonjwa wa homa ya nyani unaenea kwa kasi sana ulimwenguni kama magonjwa
ya zinaa.
kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 22, 2022 kutokana na ugonjwa huo kuenezwa
kwa mgusano wa karibu na hivyo kuwapata watu wengi ulimwenguni tangu kuripotiwa
kwa ugonjwa huo.
"Kinachoonekana kutokea sasa ni kwamba imeingia katika idadi ya watu kama njia ya ngono, katika mfumo wa uzazi, na inaenezwa kama magonjwa ya zinaa, ambayo yameongeza maambukizi yake duniani kote," David Heymann alisema.
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa lilisema, kufikia Jumamosi, kesi
92 zilizothibitishwa na kesi 28 zinazoshukiwa za ugonjwa wa homa ya nyani,
ziliripotiwa kutoka nchi 12 ikiwemo; Uingereza, Hispania na Marekani. Shirika
hilo liliongeza kuwa, litatoa mwongozo na mapendekezo zaidi katika siku zijazo
kwa nchi mbalimbali juu ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Homa ya nyani ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unapatikana sehemu za Afrika
Magharibi na Kati.
Ingawa ni ya familia ya virusi sawa na ndui, dalili zake ni kali zaidi.
Kwa kawaida watu hupona ndani ya wiki mbili hadi nne bila kuhitaji kulazwa
hospitalini, lakini maradhi hayo huwa hatari.
Ufahamu Ugonjwa Mokeypox
Monkeypox
iko kiasi gani?
Monkeypox
husababishwa na virusi vya monkeypox, kirusi wa familia moja ya virusi vya
ndui, ingawa sio kali sana na wataalamu wanasema uwezekano wa kuambukizwa ni
mdogo.
Inatokea zaidi
katika sehemu za nchi za Afrika ya kati na magharibi, karibu na misitu ya
kitropiki.
Kuna aina mbili kuu
za virusi - Afrika Magharibi na Afrika ya Kati.
Wagonjwa wawili kati
ya walioambukizwa nchini Uingereza walisafiri kutoka Nigeria, kwa hivyo kuna
uwezekano kwamba wanaugua aina ya virusi vya Afrika Magharibi, ambayo kwa
ujumla ni ndogo, lakini hii bado haijathibitishwa.
Kisa cha tatu
kilikuwa mfanyakazi wa afya ambaye alipata virusi kutoka kwa mmoja wa wagonjwa.
Kesi nne za hivi
karibuni - tatu huko London na moja kaskazini-mashariki mwa Uingereza - hazina
uhusiano wowote unaojulikana, au historia yoyote ya kusafiri. Inaonekana
walipata maambukizi Uingereza.
UKHSA inasema mtu
yeyote aliye na wasiwasi kwamba anaweza kuambukizwa anapaswa kuona mtaalamu wa
afya, lakini awasiliane na wataalamu wa afya kabla ya kufika kituo cha afya.
Dalili
ni zipi?
Dalili za awali ni
pamoja na homa, kuumwa na kichwa, uvimbe, maumivu ya mgongo, kuuma kwa misuli
na udhaifu wa mwili kwa ujumla.
Mara baada ya homa,
upele unaweza kutokea, mara nyingi huanza kwenye uso, kisha kuenea kwa sehemu
nyingine za mwili, kwa kawaida viganja vya mikono na nyayo za miguu.
Upele, ambao unaweza
kuwasha sana, hubadilika na kupita hatua tofauti kabla hatimaye kutengeneza
kipele, ambacho hutumbuka baadaye. Vidonda vinaweza kusababisha makovu.
Maambukizi kawaida
huisha yenyewe na hudumu kati ya siku 14 na 21.
Je,
unaipataje?
Monkeypox inaweza
kuambukizwa wakati mtu yuko karibu na mtu aliyeambukizwa. Virusi vinaweza
kuingia mwilini kupitia ngozi iliyo na jeraha au michubuko, kwa njia ya
upumuaji au kupitia macho, pua au mdomo.
Inaweza pia kuenezwa
kwa kugusana na wanyama walioambukizwa kama vile nyani, panya na kindi , au kwa
vitu kama vile matandiko na nguo.
Je,
ni hatari kiasi gani?
Kesi nyingi za virusi ni hafifu, wakati mwingine
hufanana na tetekuwanga, na huisha yenyewe ndani ya wiki chache.
Ugonjwa huu wakati fulani unaweza kuwa mkali zaidi,
hata hivyo, na imeripotiwa kusababisha vifo Afrika Magharibi.
Mlipuko uko kwa kiasi gani?
Virusi hivyo viligunduliwa kwa mara ya kwanza kwa
tumbili aliyefungwa na tangu 1970 kumeripotiwa milipuko ya hapa na pale katika
nchi 10 za Afrika.
Mwaka wa 2003 kulitokea mlipuko nchini Marekani,
mara ya kwanza ugonjwa huo kuonekana nje ya Afrika. Wagonjwa walipata ugonjwa
huo kutokana na kuwasiliana kwa karibu na mbwa wa mwituni ambao walikuwa
wameambukizwa na aina mbalimbali za mamalia wadogo walioingizwa nchini. Jumla
ya kesi 81 ziliripotiwa, lakini hakuna iliyosababisha vifo.
Mnamo 2017, Nigeria ilikumbwa na mlipuko mkubwa
zaidi kuwahi kurekodiwa, takriban miaka 40 baada ya nchi hiyo kuwa na visa
vyake vya mwisho vilivyothibitishwa vya monkeypox. Kulikuwa na kesi 172
zilizoshukiwa za monkeypox, na 75% ya waathiriwa walikuwa wanaume wenye umri wa
kati ya miaka 21 na 40.
Matibabu ni nini?
Hakuna matibabu yake, lakini milipuko inaweza
kudhibitiwa kwa kuzuia maambukizi.
Chanjo dhidi ya ndui imethibitishwa kuwa na ufanisi
wa 85% katika kuzuia monkeypox, na bado wakati mwingine hutumiwa.
Je, umma unapaswa kuwa na wasiwasi?
Wataalamu wanasema hatari kwa umma ni ndogo.
Prof Jonathan Ball, profesa wa stadi za virusi, Chuo
Kikuu cha Nottingham, alisema: "Ukweli kwamba ni mtu mmoja tu kati ya watu
50 walioambukizwa unaonesha jinsi virusi hivyo havina uwezo wa kuambukiza.
Dk Nick Phin, naibu mkurugenzi, Huduma ya Kitaifa ya
Maambukizi katika Afya ya Umma Uingereza (PHE), aliongeza: "Ni muhimu
kusisitiza kwamba monkeypox haisambai kwa urahisi kati ya watu na hatari ya
jumla kwa umma ni ndogo sana."
PHE inafuatilia wale ambao wamekuwa na mawasiliano
ya karibu na mgonjwa ili kutoa ushauri na kuwafuatilia inapobidi.
Habari
hizi ni kwa msaada wa mashirika ya kimataifa ikiwamo BBC


No comments
Post a Comment