Zinazobamba

TALGWU yakanusha Taarifa za Gazeti la Jamhuri lililoandika Kuhusu Upigaji wa Fedha za Chama


Katibu Mkuu wa TALGWU akizungumza na wanahabri

Na Mussa Augustine.

Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Nchini(TALGWU) kimekanusha habari zinazodaiwa kuwa za upotoshaji zilizotolewa na gazeti la Jamhuri kwa madai ya kupigwa kwa fedha za chama hicho kwenye zabuni ya kutengeneza sare za Mei mosi 2022 pamoja na utata wa manunuzi ya gari la chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Chama hicho Rashid Mtima amesema taarifa zilizochapishwa na gazeti la Jamhuri la tarehe 10 -16  mwezi huu toleo namba 554 lililosomeka kuwa "Fedha za TALGWU zapigwa"ni  taarifa za upotoshaji  kwa umma na wanachama wao ili kuvuruga mshikamano uliopo nakuleta chuki kati ya wanachama na uongozi.

Kuhusu uchapishaji wa sare za Mei mosi 2022 ,Katibu Mkuu huyo amesema kwamba mchakato wa manunuzi ya sare za Mei mosi mwaka huu ulizingatia taratibu zote za manunuzi nakumpata mzabuni ambaye kampuni ya Savana General Merchandise ambaye alipewa kazi ya uchapaji na usambazaji wa sare elfu themanini(80,000) zenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 1.1 lakini baada ya mapokezi ya sare hizo zikagundulika kuwa na mapungufu ya ubora ndipo ofisi ilipochukua maamuzi ya kumjulisha mzabuni huyo na kumtaka asimamishe zoezi la usambazaji.

Katibu Mkuu wa TALGWU Bw.Rashid Mtima amendelea kusema kwamba mzabuni huyo amelipwa kiasi Cha shilingi milioni mia saba(700) pekee Kwa mujibu wa mkataba na siyo bioni 1.1 kama ilivyoripotiwa na Gazeti la Jamhuri.

"Hata hizi milioni mia saba hazijapotea kuna taratibu zinafuatwa,kwasababu mzabuni hajakamilisha baadhi ya makubaliano kwenye mkataba hivyo tunafuatilia hatua kwa hatua,lazima tukae nae tuelewane tusipoelewana kuna mambo ya kisheria ,hii ni taasisi hivyo ina mifumo yake"amesisitiza

Kuhusu unuzuzi wa gari Bw.Mtima amewambia waandishi wa habari kwamba katika Gazeti la Jamhuri la tarehe 24 mwaka huu toleo namba 556 lililosomeka kuwa "Utata ununuzi Magari TALGWU" taarifa hiyo ni mwendelezo wa kukichafua na kuzua taharuki Kwa wanachama wake bila sababu za msingi.

" Madai ya gezeti hilo kwamba fedha za ununuzi wa gari ya Katibu Mkuu zilitosha kununua gari jipya lakini likanunuliwa la mtumba, hivyo napenda ieleweke kwamba mchakato wa ununuzi wa gari hili ulizingatia taratibu zote za kanuni za manunuzi ya chama toleo la mwaka 2018 na TALGWU haikuwahi kudhamilia kununua gari jipya kwa kuwa uwezo wa kutenga milioni mia nne( 400) Kwa ajili ya kununua gari la katibu mkuu hatuna"amesema Mtima.

Nakuongeza kuwa "Chama  kilitenga pesa za kununua gari la mtumba kiasi cha shilingi milioni mia moja na themanini (180) yakununua gari aina ya Toyota Land cruiser V8 nasio kama ilivyoripotiwa kwamba imenunuliwa kwa kiasi cha shilingi milioni mia nne nakwamba TALGWU hufanya manunuzi kwa kuzingatia uwezo wa kifedha uliopo kwa wakati husika na kanuni zake hazilazimishi chama kununua Magari mapya( 0 Kilometa). 

Hata hivyo amesema kwamba bado wanachama wa TALGWU wanaimani kubwa na uongozi wake kwani wanaziona juhudi za uongozi wa chama katika kutetea haki na maslahi yao wakiwa kazini hivyo chama kimejipanga kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya Gazeti la Jamhuri kuendelea kutoa taarifa zenye lengo la kukichafua chama na kukidhalilisha.

No comments