SERIKALI YAJA NA MPANGO MKAKATI WAKUSADIA WATU WENYE UHITAJI WA VIFAA TIBA SAIDIZI.
Na. Dominic Haule
Serikali kupitia Wizara Afya imesema kuwa imejipanga kuhakisha wanaweka utaratibu wa huduma za watu wenye changamoto ya Viungo saidizi waingizwe katika mfumo wa Bima ya Afya (NHIF)
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za Tiba kwa Hospital zote hapa nchini Luteni Kanali Dokta Pius Horumpende Wakati wa Mkutano uliyowakutanisha wadau mbalimbali wanajishughulisha na uuzaji na utengenezaji wa Vifaa Tiba saidizi wa watu wenye Ulemavu wa Viungo.
"amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakisha kuwa wananchi wanapata huduma hii muhimu kwa Unafuu hasa kwa watu wenye uhitaji wa adha hiyo ya Vifaa Tiba saidizi vya Viungo vya watu hao".
Serikali itaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo kutoa nafuu kwa vifaa muhimu kama hivi vya vifaa tiba Viungo ili kuhakisha wananchi wanapata huduma njema na wananchi kufurahia huduma za hospital zinazotolewa hapa nchini.
Naye Rais wa chama Cha Watu wanao toa huduma ya Vifa Tiba na Viungo Saidizi Bi. Leah Baiki amesema kuwa mkutano huo umewakutanisha wadau tofauti wanao jihusisha na Utengenezaji na wauzaji wa Vifaa tiba vya Viungo saidizi ikiwa lengo ni kuhakisha wanapeana uzoefu na kutoa elimu kwa Jamii juu ya huduma hizo wanazozitoa.
Ameongeza kuwa mkutano huo umeendana na maonesho ya kuonyesha shughuri zao wanazozitoa kwa wananchi ili waweze kufahamu huduma hizo sambamba na kufahamiana kama wadau wa sekta hiyo muhimu katika nchi.
Kwa upande wao washiriki wa Maonesho Akiwemo Bwana Salmin Hausi Mkwachu, Prosthetist orthotist, Mtaalam viungo na vifaa tiba saidizi kutoka Tasisisi ya Harowin Orthopaedic Rehabilitation Clinic,
Cliniki ya viungo na vifaa tiba saidizi Harowin Mshiriki wa Maonesho hayo amesema kuwa kama Wadau wa Shiriki wa Maonesho hayo wameiomba Serikali kuhakikisha wanawasaidia katika kuwapunguzia tozo za Vifaa Tiba saidizi vya Viungo vya Watu wenye changamoto ya Ulemavu kwa kufanya hivyo watasadia jamii na kumudu bei ya ununuzi wa Vifaa hivyo hasa kwa wale wenye changamoto hiyo.
Aidha kama Tasasia na Wadau wengine wataendelea kutoa Ushirikiano wao wa dhati kwa Serikali katika kutoa huduma hii kwa Wananchi hasa pale wanapo hitaji ili jamii hasa wenye changamoto hiyo ya Ulemavu waweze kupatiwa huduma kwa kiwango Cha juu mno.
Ameongea kuwa maonesho hayo ya Siku tatu yanayo endelea Makumbusho ya Taifa Jiji Dar es salaam yenye lengo la kuelimisha jamii juu ya Vifaa Tiba saidizi vya Viungo vya Watu wenye changamoto pamoja na kuwaongezea Uelewa wananchi juu ya Vifaa hivyo.


No comments
Post a Comment