Taasisi ya Wanawake Laki Moja yamuunga Mkono Rais Samia kwa Utendaji Wake wa Kazi.
Balozi wa Utalii na Mkurugenzi wa Miradi wa Taasisi ya Wanawake laki Moja Nangasu Warema(katikati) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani)kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Vicky Kamata na Kulia kwake ni Mkurugenzi wa haki za wanawake wa Taasisi hiyo Josephine Matiro.
Taasisi isiyokua ya Kiserikali ya Wanawake Laki Moja (Women 100,000) imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuongeza kima cha chini cha Mshahara kwa asilimia 23.3 ambapo hatua hiyo inawafanya wafanyakazi kuwa na morali yakufanya kazi. \ Pia taasisi hiyo imesema kwamba rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha ujasiri wa Kipekee,ubunifu na uthubutu katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizotokea Nchini na Duniani Kwa ujumla tangu achukue uongozi wa Nchi mwezi Machi mwaka Jana. Pongezi hizo zimetolewa Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Vicky Kamata wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amesema kwamba rais Samia Suluhu Hassan amefanya Mambo mengi Kwa muda huu wa uongozi wake ikiwemo kuongeza mishahara,kupandisha madaraja Kwa Watumishi wa umma,kulipa malimbikizo ya mishahara pamoja na kulipa mafao ya wastaafu Kwa wakata. "Serikali imepanga kutumia kiasi Cha shilingi trilioni 9.7 katika mwaka wa fedha ujao wa 2022 /23 Kwa ajili ya kugharamia malipo ya Mishahara ya Watumishi wa umma,hili ni ongezeko la shiringi trilioni 1.59 ukilinganisha na Bajeti ya 2021/2022, ongezeko la kima Cha chini Cha Mishahara pamoja na kupandishwa Kwa madaraja Kwa Watumishi wa umma siyo Jambo jema Kwa Watumishi wa umma pekee bali Taifa zima" amesisitiza Vicky Kamata. Kuhusu Kupanda kwa Bei ya Mafuta Vicky Kamata amesema kwamba rais Samia Suluhu Hassan amechukua hatua za kizalendo na ujasiri wa kipekee nakutoa maelekezo Kwa serikali yake kuchukua hatua za dharura kupunguza makali ya ongezeko la Bei ya Mafuta nchini kabla ya mwaka ujao wa fedha wa 2022/2023. " Badala ya kusubiri hatua za kikodi kwenye bajeti ijayo ya serikali ambayo utekelezaji wake utaanza Julai 1,2022 rais Samia ameagiza kuwa ahueni itafutwe mapema zaidi Kwa kutoa maelekezo kwamba katika kipindi hiki kabla hatujafikia mwaka mpya wa fedha,Serikali ijibane na ijinyime na itolewe ruzuku ya shilingi bilioni mia moja Kwa ajili ya kupunguza Bei za Mafuta hapa Nchini" amesesma Vicky. Kwa upande wake Mkurugenzi wa haki za Wanawake wa Taasisi hiyo Josephine Matiro amesema kuongezwa Kwa Mishahara kutasaidia kuwepo Kwa mzunguko wa fedha,Biashara na Uchumi wa Nchi kukua ambapo siyo Watumishi pekee watakao nufaika na hatua hiyo bali hata Watanzania wasiokuwa Watumishi. " Tuna miaka saba hatujaongezwa mishahara,rais Samia tarehe 14 Mei 2022 taarifa ilitolewa na ikulu kua ameridhia mapendekezo ya kuongeza mishahara,ikiwemo kima Cha chini Kwa Watumishi wa umma Kwa asilimia 23.3 na hivyo kuibua shangwe kubwa ,ongezeko hili ni kubwa kuwahi kutokea Nchini Kwa kipindi kirefu sana" amesema Bi.Josephine. ![]() Akizungumzia kuhusu filamu ya kutangaza vivutio vya Utalii ( Royal Tour) Balozi wa Utalii na Mkurugenzi wa Miradi wa Taasisi ya Wanawake laki Moja Nangasu Warema amesema kwamba jitihada kubwa za uthubitu wa kutangaza vivutio vya Utalii kupitia filamu nakwamba haijawahi kutokea tangu Nchi ipate Uhuru miaka sitini iliyopita lakini rais Samia amefanya filamu hiyo ndani ya kipindi Cha uongozi wake wa mwaka mmoja. " Bila kumung'unya maneno Royal Tour ni ubunifu na jitihada kubwa za kutangaza fursa za Utalii na Uwekezaji Nchini ambazo sote tunafahamu namna ambavyo Nchi jirani zemekuwa zikitumia mabilioninya fedha kutangaza Utalii wao Duniani huku Tanzania ikiachwa nyuma hadi kupelekea baadhi ya watu huko nje kulaghaiwa kuwa mlima Kilimanjaro na Serengeti ziko Nchi jirani na siyo Tanzania" amesema Balozi wa Utalii Nangasu.
|


No comments
Post a Comment