Zinazobamba

NIMR yazindua Maabara ya Utafiti wa Vianasaba Vya Ugonjwa wa Malaria.

Na Mussa Augustine.

Serikali kupitia Taasisi yake ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)imesema itahakikisha imeongeza jitihada za kutokomeza Ugonjwa hatari wa Malaria ambao umendelea kuwa tishio na kusababisha watu wengi kupoteza Maisha.
Mganga Mkuu wa Serikali Dr.Aifello Sichalwe.
Akizungumza  Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maabara ya Kufuatilia Vinasaba vya Ugonjwa wa Malaria Mganga Mkuu wa Serikali Dr.Aifello Sichalwe amesema kwamba Maabara hiyo ni moja ya mkakati wa Wizara ya Afya kupitia Mpango wa kudhibiti Malaria Kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI).

Aidha amesema kwamba Mradi huo wa Maabara ya Ufuatiliaji wa Vinasaba vya Malaria una lengo la kupata ushahidi wa kina juu ya chanzo kinachosababisha ugonjwa wa Malaria nakwamba utasaidia wataalamu wa masuala ya tafiti kupata suluhisho la Kukabiliana na ugonjwa wa Malaria.

"Utafiti huu wa Vinasaba vya Malaria niwa awamu ya kwanza kutekelezwa hapa Nchini ,na unafadhiliwa na wadau wetu wa maendeleo ikiwemo Umoja wa Ulaya(UN) na tunawaomba waendelee kufadhili ,pia tunaendelea kufanya mazungumzo na wadau wengine waweze kufadhili ile uwe endelevu nakufikia lengo tulilokusudia" amesema Dr.Sichalwe.

Aidha Dr.Sichalwe ameendelea kufafanua kwamba Utafiti huo utasaidia kuwajengea uwezo NIMR Kwa kuzalisha takwimu za Vinasaba vya Maleria hapa Nchini nakuzichakata Kisha wizara ya Afya itazitumia kufanya maamuzi ikiwemo kuandaa miongozo,kutunga sera  nakutekeleza mikakati mbalimbali yakupambana na Malaria huku wakiwa na ushahidi wa kisayansi.
Awali Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu( NIMR) Dr.Khadij Malima amesema kwamba utafiti wa Vinasaba vya Ugonjwa wa Malaria umeanza tangu Mwezi Mei 2020 na utakamilika Mwezi Oktoba 2023 ambapo Kwa sasa umetekelezwa katika Mikoa kumi na tatu Nchini kote.

Aidha ameitaja Mikoa hiyo kuwa ni pamoja Dar es salaam,Morogoro,Dodoma,Manyara,Pwani,Songwe,Ruvuma,Tabora,Tanga,Kagera,Mtwara,Kigoma,Mara.
nakusema kwamba wasimamizi Wakuu wa utafiti huo wa Vinasaba vya Malaria ni Waganga Wakuu wa Mikoa pamoja Afisa afya.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia ufunguzi wa Maabara ya utafiti wa Vinasaba vya Ugonjwa wa Malaria uliyofanyika katika Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIMR Mkoani Dar es salaam.

No comments