Zinazobamba

Gazeti la Tanganyika Tanzania lapewa onyo na Mahakama ya Kisutu kutoendelea kukichafua Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

Leo tarehe 18/05/2022 Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi -Kisutu, Jijini Dar es salaam imetoa amri ya zuio kwa wamiliki na wachapishaji wa gazeti la Tanganyika Tanzania ambao ni Kinarani Co.& General Publishers kutokuendelea kuchapisha Habari zenye Mlengo wa Kukichafua Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ambacho kimejijengea heshima yake  kwa miongo mingi sasa. 

Amri hiyo imetolewa na Mahakama hiyo Mbele ya Mh. Kyaruzi  ambapo Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kupitia Kesi Namba 247 ya Mwaka 2021 kiliwakilishwa  na jopo la mawakili kutoka AVIS LEGAL  akiwemo Wakili Hosea Chamba, Hamza Jabir na Henry Mwinuka , wakati upande wa pili ukiwakilishwa na Wakili Ashraf Muhidin ambae alikuwa ameshika mikoba ya wakili Katala Karimba  anayewawakilisha walalamikiwa Kinarani Co. & General Publishers.

No comments