Zinazobamba

Makumbusho ya Taifa Yaiomba Jamii Kuwa na Ushirikiano wa Kutoa Taarifa Sahihi za Vielezo Vya Mali Kale.

Na Mussa Augustine.

Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw.Achiles Bufure ameiomba jamii kuwa na ushirikiano wa kutoa taarifa za vielelezo vya mali kale ili kuwezesha kufanya uhifadhi wa mali kale hizo katika Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijavyo.
Wanafunzi kutoka shule za Sekondari Jitegemee,Benjamini,Osterbey,Makongo wamehudhulia katika siku ya Makumbusho Duniani iliyofanyika katika Makumbusho ya Taifa yaliyopo Posta jijini Dar es salaam,ambapo wameshiriki katika program mbalimbali zilizoandaliwa na Makumbusho ya Taifa katika maadhimisho hayo.
Mkurugenzi huyo ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam Wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye Maadhimisho ya siku ya Makumbusho Duniani mwaka 2022, yaliyobeba kauli mbiu isemayo "Nguvu ya Makumbusho",ikiwa na maana kwamba Makumbusho ya Taifa inasimamia misingi mikuu ambayo ni Utafiti,Elimu na Uhifadhi.

Aidha amesema kwamba Makumbusho ya Taifa inakumbwa na changamoto mbalimbali katika upatikanaji wa vielelezo vya mali kale ikiwemo wananchi wa makabila mbalimbali kushindwa kutoa ushirikiano wa vielelezo vya Mila na tamaduni zao ili kuwezesha kupata mali kale na kuhifadhi kwenye Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni.

" Tanapata changamoto ya kupata taarifa sahihi,makabila mengi yanaweka siri hayapendi kutoa taarifa ,hii ni changamoto kubwa kwetu kupata vielelezo vya mali kale ili tuweze kuhifadhi kwenye makumbusho kwa ajili ya kizazi kilichopo na kijacho " amesema Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni  bw, Bufure.

Aidha Bw.Bufure amesema kwamba kwa sasa wanafunzi wapatao mia nne hadi mia sita kwa wiki  wanatembelea makumbusho ya Taifa,huku idadi    ya wananchi wengine wanaotembelea Makumbusho hayo kwa ajili ya kujionea vielelezo vya mali kale  ikizidi kuongezeka,ambapo ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa jamii kupenda kutembelea makumbusho ya Taifa.

Kwa upande wake Mwalimu wa Shule ya Sekondari Jitegemee ya jijini Dar es salaam Brighton Mbasha amesema kwamba Makumbusho ya Taifa inawasaidia wanafunzi kujifunza mambo mengi akitolea mfano histori ya Afrika,Biashara za utumwa nakwambia ni sehemu ya chimbuko zuri kwa wanafunzi kupata vielelezo vya mambo ya kale.

Muhsini Pembe mwanafunzi wa Sekondari Benjamini na Unosye Atufigwege wa shule ya Sekondari Jitegemee kwa niaba ya wanafunzi wenzao wamewambia waandishi wa habari kwa nyakati tofauti kuwa Makumbusho ya Taifa ni sehemu ya kupata elimu kwa vitendo kuhusu vielelezo vya mambo ya kale nakwambia wao ni mawakala wa kutoa elimu kwa wanafunzi wenzao pamoja na jamii kwa ujumla.


No comments