Dkt.Mpango awataka Watafiti Kufanya Tafiti Zenye Kuleta Suluhisho ya Changamoto Zinazoikumba Jamii.
Na Mussa Augustine.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Philip Mpango amewataka watafiti wa Magonjwa Mbalimbali kuhakikisha wanafanya tafiti zitakazoleta suluhisho Kwa Jamii kuhusu changamoto Mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyo ya kuambukiza.
Dr.Mpango ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es salaam wakati akifungua kongamano la kisayansi la 31 lililoandaliwa na NIMR,ambapo limewakutanisha Watafiti Mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi ikiwa lengo ni kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya katika utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi.
Aidha ameendelea kusema kwamba tafiti zinazofanywa na Watafiti zinaisadia Serikali kuchukua maamuzi ya kisera katika kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayojitokeza Kwa Jamii akitolea mfano magonjwa ya mripuko, na magonjwa ya kuambukiza kama vile janga la UVICO 19 lililosumbua Dunia nakusabisha vifo vya watu na uchumi kuporomoka.
Katika hatua nyingine Makamu huyo wa rais Dr.Philip Mpango amekabidhi tuzo za NIMR Kwa Watafiti sita,pamoja nakuwazawadia shilingi milioni moja Kwa kila mmoja wao, nakutumia fursa hiyo kumuagiza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuanzisha tuzo ya watafiti vijana itakayokuwa ikitolewa kila mwaka na Wizara hiyo ikiwa lengo ni kufanya motisha Kwa watafiti hao.
Nae Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameiagiza NIMR kufanya pia tafiti za tiba asili kwani asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia tiba hizo pasipokua na elimu yakufahamu kama zinaweza kuwa na madhara ya sumu nakusababisha athari zakiafya.
"Kwa mwaka 2018 wasichana walio na umri wa kuanzia miaka 12 hadi 14 walikuwa wanachanjwa chanjo ya Saratani ya Mlango wa shingo ya kizazi,ambapo ilikua dozi mbili nakwamba walichanjwa asilimia 70 ya wasichana katika awamu ya kwanza lakini awamu ya pili wakarudi wasichana wachache kuchanja chanjo hiyo, hali ambayo iliifanya NIMR ifanye utafiti wa chanjo hiyo na kubaini kua chanjo moja waliopatiwa inatosha hivyo kuanzia tarehe 1 mwezi wa Saba mwaka huu itaanza kutolewa chanjo moja pekee ya Saratani ya shingo ya uzazi" amefafanua Waziri Ummy Mwalimu
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa na Tiba ( NIMR) Prof.Yunus Mgaya amemuhakikishia Makamu wa rais Dr.Philip Mpango pamoja na Waziri wa afya kuwa utafiti wa chanjo ya Ugonjwa wa UVIKO 19 unaendelea kufanyiwa nakwamba majibu ya utafiti huo yatakamilika mwishoni mwa mwaka huu.
"Kuanzia mwezi wa kumi na mbili tulianza kufanya tafiti ya chanjo za corona ,tuna dozi za kutosha za chanjo ya corona kilichobaki nikuwandiakisha wananchi kwenye vituo vyetu vya Dar es salaam na Mbeya ,hivyo tunafanya tafiti hizi Kwa awamu,tutatoa majibu ya tafiti mwisho wa mwaka huu" amesema Prof.Yunus Mgaya.
Kongamano hilo linatarajiwa kufikia kilele Mei 19 mwaka limebeba ujume usemao" Ushiriki wa sekta mbalimbali katika afya kufikia huduma ya afya wote" ambapo limehudhuliwa na wataam mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi pamoja na watunga sera.


No comments
Post a Comment