PSPTB yawataka waajiri kuwaondoa kwenye kitengo Maafisa Wasio na Sifa za Kitaaluma.
Na Mussa Augustine.
Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB) imewataka waajiri wote Sekta ya Umma na Binafsi kuwaondoa kwenye kitengo Cha Ununuzi na Ugavi Maafisa wote wasio na sifa za Kitaalam Kwa mujibu wa muongozo wa usajili wa PSPTB na muundo wa Utumishi wa kada zilizopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango waraka namba 3 wa mwaka 2015.
| Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya PSPTB, Bw. Godfred Mbanyi akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam. |
Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Bw. Godfred Mbanyi wakati akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam nakusema kwamba Bodi hiyo imebaini bado kuna Waajiri Wanaajiri watu kufanya kazi za Ununuzi na Ugavi bila Usajili wa PSPTB hali ambayo ni kinyume Cha sheria.
"Katika kutekeleza jukumu hilo kisheria, PSPTB imebaini bado kuna Waajiri Wanaajiri watu kufanya kazi za Ununuzi na Ugavi bila usajili wa Bodi yetu,kupitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya ununuzi wa Umma (PPRA) zimeonyesha ukiukwaji wa sheria Kwa kitengo Cha ununuzi kuwa na Wakuu wa Vitengo wasio na sifa za kitaaluma" amesema Bw.Mbayi
Nakuongeza kwamba" Pia taarifa hizi zimebaini mapungufu makubwa kwenye ukidhi wa Sheria ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake nakupelekea hasara kwa Serikali ,hivyo PSPTB inawataka wataalamu wote wanaofanya kazi kwenye kitengo Cha Ununuzi na Ugavi kuhakikisha wanafanya kazi Kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao Kwa mujibu wa muongozo wa maadili ya kazi ya ununuzi na ugavi wa Bodi hiyo.
Aidha ameendelea kuwaagiza wataalam wa Ununuzi na Ugavi wa Sekta binafsi na Umma kufanya kazi Kwa weledi na kutoa ushauri Kwa umakini bila hofu ili kupata thamani ya Fedha.
" Kuanzia Mei 17 tunaanza kutoa Elimu Kwa Umma kupitia vyombo vya habari,tunaomba pia Waandishi wa habari mtusaidie kufikisha Elimu hii ili tuweze kudhibiti upotevu wa fedha nyingi ambazo zimekua zikipotea kutokana na kukosekana Kwa weledi wa kazi Kwa baadhi ya Wafanyakazi wa Manunuzi na Ugavi" amesisitiza Mkurugenzi Mtendaji huyo wa PSPTB.
No comments
Post a Comment